Simba wamnasa winga kutoka TP Mazembe

Simba wamnasa winga kutoka TP Mazembe

02 July 2019 Tuesday 13:35
Simba wamnasa winga kutoka TP Mazembe

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

WINGA wa kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Deo Gracia Kanda Mukoko amejiunga rasmi  na klabu ya Simba ya Dar es Salaam akitokea  TP Mazembe ya Lubumbashi.

Kanda Mukoko amesaini mkataba wa mwaka mmoja kukipiga Msimbazi akitokea TP Mazembe ambapo alikuwa mmoja wa wachezaji ambao waliiwezesha kushinda Ubingwa wa Afrika mwaka 2009, 2010 (aliifungia goli kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Esperance) na 2013 lakini pia akiwa ameshiriki Kombe la Dunia la Vilabu mwaka 2009, 2010, 2013.

Hata hivyo taarifa ya TP Mazembe ya Juni 30,2019 imesema kwamba Kanda amekuja Tanzania kukamilisha mipango ya kujiunga na mabingwa wa Tanzania kwa mkopo wa msimu mmoja.

Hakukuwa na ufafanuzi zaidi juu ya mpango huo, lakini taarifa zisizo rasmi zinasema Simba SC wanapewa Kanda kwa mkopo baada ya kukubali kumuachia kiungo mshambuliaji, Ibrahim Ajibu iliyemsajili tena kutoka kwa mahasimu, Yanga.

Inadaiwa Simba SC wamerejeshewa fedha zao walizompa Ajibu na kupewa Kanda kwa mkopo baada ya mazungumzo ya kiungwana yaliyozaa makubaliano hayo. 

Kanda alitua kwa mara ya kwanza Mazembe mwaka 2009 na alikuwemo kwenye kikosi cha timu hiyo kilichoshiriki klabu bingwa ya dunia ya FIFA mwaka 2010, kabla ya kuhamia Raja Casablanca ya Morocco mwaka 2013.

Alicheza Morocco kwa msimu mmoja kabla ya mwaka 2014 kurejea nyumbani, DRC na kujiunga AS Vita alikocheza kwa msimu mmoja pia kisha akajiunga tena na Mazembe mwaka 2015 hadi sasa anatolewa kwa mkopo.

Updated: 03.07.2019 15:05
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
James 2019-07-12 22:55:06

karibu msimbanzi