Simba washusha kiungo hatari, Ndemla, Muzamiru matatani

Amewahi kucheza soka la kulipwa Ulaya

Simba washusha kiungo hatari, Ndemla, Muzamiru matatani

Amewahi kucheza soka la kulipwa Ulaya

14 June 2018 Thursday 13:38
Simba washusha kiungo hatari, Ndemla, Muzamiru matatani

Na Amini Nyaungo

Klabu ya Simba ikiwa imedhamiria kufanya makubwa katika soka nchini na nje ya mipaka ya Tanzania, imeendelea kuonyesha jeuri ya fedha huku ikiwa tayari kumnasa nyota yoyote kutoka sehemu yoyote katika bara la Afrika ili kuweza kutimiza lengo lake hilo.

Tetesi za usajili kutoka ndani ya klabu hiyo ya mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam zinasema kuwa jembe kutoka Gor Mahia limefikia makubaliano kwa ajiri ya kuitumikia timu hiyo.

Fransic Kahata ambaye ni mmoja ya nyota wa mabingwa hao wa nchini Kenya wanaofanya vizuri sana katika klabu hiyo na kuonyesha kiwango cha hali ya juu wakati wa mashindano yaliyomalizika hivi karibuni ya SportsPesa Super Cup.

Baada ya benchi la ufundi kumuona mchezaji huyo wameamua kurusha ndoano ili kumnasa na kwa hakika imemnasa.

Baada ya tetesi hizi wengi wanasema nafasi ya viungo kama Mzamiru Yassin pamoja na Said Ndemla itakuwaje. Wengine wakisema wakati wa kutimka umewadia.

Hata hivyo Ndemla amehusishwa na kujiunga na klabu ya Yanga ambayo ilimuhitaji tangu msimu uliopita.

Mjadala huo umekuwa mkubwa sana haswa wakidhani kuwa nafasi zao zimefika ukingoni na watafute mahali watakapoweza kwenda na kucheza kila mechi.

Kahata mwenye umri wa miaka 27 amecheza michezo 21 ya timu ya taifa ya Kenya na kuweza kufunga magoli 2 huku amejiunga na Gor Mahia msimu wa 2015 akitokea KF Tirana, klabu inayoshiriki ligi kuu huko Ulaya katika nchi ya Albania.

Azania Post

Updated: 14.06.2018 13:45
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.