Simba watoa tamko jipya juu ya Niyonzima, Juuko kuhusu Simba Day

Simba watoa tamko jipya juu ya Niyonzima, Juuko kuhusu Simba Day

10 August 2018 Friday 07:59
Simba watoa tamko jipya juu ya Niyonzima, Juuko kuhusu Simba Day

Baada ya kushindwa kutangazwa katika orodha ya wachezaji ambao walihusika na tamasha kubwa la Simba Day Agosti 8, uongozi wa klabu hiyo umefunguka juu ya Haruna Niyonzima na Juuko Murshid.

Kwa mujibu wa Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah maarufu kama Try Again, amesema kukosekana kwa wachezaji kutambulishwa katika tamasha hilo haina maana kuwa wameachana nao.

Akizungumza kupitia Radio Magic FM, Again ameeleza kuwa Juuko na Niyonzima watakuwa nao siku za usoni kwa sababu bado ni mali ya klabu huku wakiwa na mikataba.

Aidha, Try Again amewataka wanachama na mashabiki wa Simba kuipenda klabu na kuondoa hofu kwa wachezaji akiwa anaamini bado kina uwezo mkubwa wa kufanya vizuri hata wasipokuwepo.

"Kuhusu suala la Haruna Niyonzima na Juuko Murshid kutotangazwa Simba DAY jana, halimaanishi kuwa si wachezaji wetu. Wachezaji hao watakuwa nasi siku za usoni kwa maana bado ni mali yetu. Kingine wapenzi na wanachama wa Simba wanapaswa kuipenda klabu na si kuonesha hofu kwa wachezaji," alisema.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
pascal mungai kutoka qhaeshoman,mbulu -manyara@ 2019-07-18 23:09:25

Haruna tunakuomba xana ubakie simba tunakuhitaji tunakupenda sisi kama mashabiki wako na simba kwa ujumla please kaeni na viongozi muzimalize hizo tofaut zenu mambo yatakuw xaw.