Simba yaanza mawindo, kutumia jezi tatu tofauti

Simba yaanza mawindo, kutumia jezi tatu tofauti

16 July 2019 Tuesday 15:06
Simba yaanza mawindo, kutumia jezi tatu tofauti

Na mwandishi wetu.
TIMU ya Simba SC imeanza rasmi mazoezi ya kujiandaa na mashindano ya kitaifa na kimataifa msimu wa mwaka 2019/20. Pia klabu hiyo imezidua jezi mpya tatu kukidhi matakwa ya shirikisho la soka Afrika(CAF)

Ikiwa na wachezaji wake takribani wote isipokuwa watatu ambao hawakuondoka na timu hiyo jana Julai 15 kutokana na kuchelewa kupata pasi ya kusafiria(visa) wachezaji wameanza matizi asubuhi ya leo Julai, 16, 2019. katika mji wa  Rustenburg, Afrika Kusini  na yatakuwa yakifanyika mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mtendaji mkuu wa klabu hiyo, Crescentius Magori amesema klabu hiyo imepata udhamini wa kampuni ya vifaa vya michezo ya Romario itakayotoa vifaa vyote vya michezo kwa timu hiyo na kwamba sherehe za Simba Day zipo  zitafanyika Agosti 8.

"Tutakuwa na jenzi tatu, ili kukidhi masharti ya CAF, Nyeupe ni ugenini, Nyekundu ni ya Nyumbani na Kijivu ni 'neutro'''  amesema Magori

Kuelekea msimu ujao, tayari Simba SC imesajili wachezaji 11 wapya hadi sasa, ambao ni kipa Beno David Kakolanya, baki Gardiel Michael Mbaga na kiungo Ibrahim Ajibu Migomba wote kutoka Yanga SC, ambao kwa pamoja na beki wa kati, Kennedy Wilson Juma kutoka Singida United na Miraj Athuma I ‘Madenge’ kutoka Lipuli wanafanya idadi ya wachezaji watano wazawa wapya Msimbazi hadi sasa.

Wengine sita wote ni wa kigeni, Wabrazil mabeki beki Gerson Fraga Vieira ATK ya Ligi Kuu ya India na Tairone Santos da Silva kutoka klabu ya Atletico Cearense FC, mshambuliaji, Wilker Henrique da Silva kutoka Bragantino, zote za Daraja la Nne nchini Brazil na viungo Mkenya, Francis Kahata Nyambura, Msudan Sharaf Eldin Shiboub Ali Abdalrahman na winga Deo Kanda kutoka TP Mazembe ya kwao, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Pamoja na kusaini wachezaji wapya, Simba SC pia imewapa mikataba mipya wachezaji wake kadhaa wa msimu uliopita, wakiwemo kipa Aishi Manula, mabeki Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Nahodha Msaidizi, Mohammed Hussein ‘Tshabalala, Muivory Coast, Serge Wawa Pascal viungo Jonas Mkude, Mzambia Clatous Chama na washambuliaji Nahodha Mkuu, John Bocco na Meddie Kagere raia wa Rwanda.

Updated: 17.07.2019 17:48
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.