Simba yafunga pazia Ligi Kuu, yalazimishwa sare na Majimaji

Hiyo inakuwa sare ya tisa ya msimu kwa mabingwa hao wapya

Simba yafunga pazia Ligi Kuu, yalazimishwa sare na Majimaji

Hiyo inakuwa sare ya tisa ya msimu kwa mabingwa hao wapya

28 May 2018 Monday 19:43
Simba yafunga pazia Ligi Kuu, yalazimishwa sare na Majimaji

Na Habakuki Urio

MABINGWA wa soka la Tanzania Simba SC wamefanikiwa kumaliza msimu kwa kupoteza mchezo mmoja tu baada ya sare 1-1 dhidi ya Majimaji Mjini Songea.

Hiyo inakuwa sare ya tisa ya msimu kwa mabingwa hao wapya, huku ikishinda mechi 20 na kufungwa moja tu dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa.

Maji Maji FC leo walitangulia kwa bao la mshambuliaji Marcel Boniventusa Kaheza kabla ya kiungo kutoka Rwanda, Haruna Niyonzima kusawazisha kwa njia ya penalti.

Niyonzima pia alipoteza penalti nyingine ambayo ingeweza kuwapa Simba ushindi.

Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Ndanda FC imeshinda 3-1 dhidi ya Stand United kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara na kunusurika kushuka daraja.

Kagera Sugar imepata ushindi wa 2-1 mbele ya wenyeji, Lipuli FC ya Iringa Uwanja wa Samora, Tanzania Prisons imeilaza 1-0 Singida United Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Mtibwa Sugar imetoka sare ya 0-0 na Mbeya City Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro, Mbao FC imetoka sare ya 1-1 na Ruvu Shooting Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza na Mwadui FC imewapiga wenyeji, Njombe Mji FC 2-0 Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe.

Maji Maji na Njombe Mji FC ziimeshuka Daraja kutokana na tayari African Lyon, KMC, JKT Tanzania za Dar es Salaam, Coastal Union ya Tanga, Alliance Schools ya Mwanza na Biashara United ya Mara zimekwishapanda kuelekea ligi ya msimu ujao, itakayokuwa na timu 20 ambayo ni ongezeko la timu nne.

Timu

Maji Maji; Hashim Mussa, Aziz Sibo, Mpoki Mwakinyuke, Juma Salamba, Kennedy Kipepe, Hassan Khamis, Peter Mapunda, Lucas Kikoti, Jerson Tegete, Marcel Kaheza na Jaffar Mohamed.

Simba SC; Said Mohammed ‘Ndunda’, Ally Shomary, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Vincent Costa, Paul Bukaba, Muzamiru Yassin, Mohammed Ibrahim, Said Ndemla, Juma Luizio, Rashid Juma na Haruna Niyonzima.

Azania Post

Updated: 28.05.2018 20:26
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.