banner68
banner58

Simba yaifanyia Yanga unyama: Wawili wakimbilia pesa za ‘Mo’

Simba yaifanyia Yanga unyama: Wawili wakimbilia pesa za ‘Mo’

26 June 2018 Tuesday 10:04
Simba yaifanyia Yanga unyama: Wawili wakimbilia pesa za ‘Mo’

Na Amini Nyaungo

Baada ya hapo jana  kumalizana na Serge Wawa ambaye alitakiwa atue Yanga, sasa Simba imerejea tena na kuinasa saini ya mshambuliaji mahiri wa Gor Mahia Medie Kagere na sasa ala kandarasi la mwaka mmoja

Yanga walihitaji sana saini ya Kagere ambaye amefanya vizuri katika michuano ya Sports Pesa Super Cup ikishuhudia Gor Mahia ikichukua nayeye akiweka kambani magoli manne.

Klabu hiyo imeonekana ikiwa na mchezaji huyo katika ofisi za Simba huku wakala wake akithibitisha kuwa Simba walikuwa siriazi katika kuhitaji saini ya Kagere ndio maana ametua katika klabu hiyo.

“Simba walikuwa ‘serious’ sana katika kuhitaji saini ya Kagere tofauti na klabu ya Yanga ndio maana amesajiliwa hapa Simba,” amesema Gakumba.

Hii ndio kauli thabiti ya Simba ambayo mtamkaji anaanza kusema  ‘this is….. wamaliziaji wanamalizia Simbaaa; muasisi akiwa Haji Manara.

MKataba wake ni mwaka mmoja ambapo kotokana na umri wake wa miaka 31 kama atafanya vizuri Zaidi basi ataongezewa kwa mujibu wa vyambo vyetu vya habari.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.