Simba yamnasa Mbrazil mwingine

Simba yamnasa Mbrazil mwingine

25 June 2019 Tuesday 14:38
Simba yamnasa Mbrazil mwingine

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

KLABU ya Simba imemsajili mchezaji  mwingine kutoka Brazil anayecheza nafasi ya beki wa kati na kiungo mkabaji, Gerson Fraga Vieira (26) ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili na mabingwa  hao wa ligi kuu  msimu wa mwaka 2018/19. 
 
Amejiunga na timu ya Simba akitokea timu ya ATK FC ya  nchini India.

Vieira  amewahi kuwa nahodha wa timu ya Taifa ya wachezaji chini ya miaka 17 ya Brazil iliyokuwa na wachezaji maarufu kama Neymar, Philippe Coutinho, Casemiro na golikipa Alisson, pia alicheza timu ya Taifa ya wachezaji chini ya miaka 20 na alicheza klabu kadhaa za Brazil ikiwepo Grêmio.

Juni 21, 2019 pia klabu ya Simba ilimsajili mshambuliaji Mbrazil, Wilker Henrigue.

Updated: 26.06.2019 09:23
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.