Simba, Yanga uso kwa uso tena Julai 5 kwenye Kombe la Kagame

Simba, Yanga uso kwa uso tena Julai 5 kwenye Kombe la Kagame

05 June 2018 Tuesday 13:28
Simba, Yanga uso kwa uso tena Julai 5 kwenye Kombe la Kagame

Na Amini nyaungo

Baada ya ligi kuu bara kumalizika mechi za Yanga na Simba zinakuwa nadra sana kutokea, labda kuwepo na mashindano ya kombe au mashindano maalumu.

Sasa Shirikisho la soka la nchi za Afrika Mashariki na kati kupitia mashindano yake ya kombe la Kagame ambalo ni mahsusi kwa ajili ya vilabu vya soka katika eneo hilo, Watanzania watashuhudia mchezo mkali baina ya Yanga na Simba Julai 5, 2018 hapa Dar es Salaam mara baada kupangwa katika kundi moja la ‘D’.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali kutokana na upinzani baina ya timu hizo pindi zinapokutana, na mara ya mwisho timu hizo zilipokutana katika ligi, Simba ilifanikiwa kushinda kwa bao 1-0 ambalo liliwekwa kimiani ni kiungo mahiri wa Tanzania Erasto Nyoni.

Yanga haijawahi kushinda mchezo wowote katika ligi dhidi ya Simba tangu mwaka 2016, hivyo itakuwa kama kisasi pamoja na burudani ya aina yake.

Kuna uwezekano pia wakakutana tena endapo watafanikiwa kupita katika makundi yao, kwenye nusu fainali au hata fainali.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.