Simba yatoa tamko juu ya mashabiki wake juu ya Taifa Stars v Uganda Cranes

Simba yatoa tamko juu ya mashabiki wake juu ya Taifa Stars v Uganda Cranes

01 September 2018 Saturday 09:02
Simba yatoa tamko juu ya mashabiki wake juu ya Taifa Stars v Uganda Cranes

Uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa Ofisa Habari wake, Haji Manara, umesema sakata la wachezaji wake na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeshamalizika hivyo amewaomba watanzania wote waisapoti timu hiyo.

Kauli ya Manara imekuja kufuatia Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike kuwaondoa wachezaji 6 wa Simba baada ya kuchelewa kuripoti kambini, lakini baadaye alikutana na kuzungumza nao kisha kuwasamehe.

Kutokana na kitendo cha Amunike kuwasamehe wachezaji hao, Manara amewaomba watanzania wote wakaipe sapoti timu ya taifa itakapocheza na Uganda hasusani waliopo Kanda ya Ziwa.

Ofisa huyo amesema hakuna haja ya kuitenga timu kutokana na na baadhi ya mashabiki wa Simba kuibuka na kueleza wataisaliti kwa kuipa sapoti Uganda baada ya kupatwa na hasira sababu za wachezaji wao kuondolewa.

Stars itacheza na Uganda Septemba 8 huko Kampala ukiwa ni mchezo wa kufuzu kuelekea fainali za AFCON 2019.

Updated: 01.09.2018 09:09
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.