Simba yatoa tamko juu ya mwamuzi atakayechezesha mechi yao dhidi ya Yanga

Simba yatoa tamko juu ya mwamuzi atakayechezesha mechi yao dhidi ya Yanga

27 September 2018 Thursday 07:06
Simba yatoa tamko juu ya mwamuzi atakayechezesha mechi yao dhidi ya Yanga

Baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumtangaza Jonesia Rikiyaa kama mwamuzi atayaechezesha mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga Jumapili ya wiki hii, uongozi wa Simba umesema ni vema akafuata sheria 17 za mchezo wa soka.

Simba wamesema ni haki kwao kumkosoa pale anapokosea na pia kusifia pale inapotokea amefanya vizuri kwa kuchezesha vema bila kuvunja sheria ndani ya dakika 90.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, ameeleza kuwa wao hawana tatizo na Waamuzi wote waliotangazwa na badala yake wakiomba tu mchezo uchezeshwe kwa haki.

Manara amesema mamuzi ya TFF kuwachagua waamuzi hao yako sahihi na wala hawawezi kuyaingilia kwa maana majukumu yao kama timu ni kucheza mpira na si vingine.

"Hatuwezi kuwaingilia TFF na kuzungumzia zaidi hilo, kifupi tunaomba tu mchezo uchezeshwe kwa haki na kwa kuzingatia sheria 17 za mchezo wa soka bila kuvunjwa" alisema Manara.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.