Stars warejea, waziri Mwakyembe awapokea

Stars warejea, waziri Mwakyembe awapokea

06 August 2019 Tuesday 10:45
Stars warejea, waziri Mwakyembe awapokea

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amewaongoza watanzania kuipokea timu ya taifa ya soka ya Kilimanjaro Stars.

Stars wamerejea nchini mapema leo Agosti 6,2019 ikitokea Kenya baada ya kuiondoa timu ya taifa ya soka ya Kenya kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani kwa mikwaju ya penati 4-1.

Sasa Stars inajipanga kukutana na Sudan katika mechi nyingine ya kufuzu mashindano ya Afrika kwa wachezaji wanaochezea ligi za ndani ya CHAN 2020 itayochezwa nchini Cameroon

PICHANI JUU:Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kulia) akisalimiana na baadhi ya wachezaji wa Kilimanjaro Stars mara baada ya kutua nchini wakitokea Kenya

PICHANI CHINI, Waziri Dk Mwakyembe (kulia) akifurahia jambo na viongozi wa Timu ya Taifa ya Kilimanjaro Stars mara baada ya kuwapokea wakitokea nchini Kenya walikowa katika mchezo wa marudiano na Timu ya Taifa ya Kenya katika mashindaon ya CHAN, Tanzania ilishinda 4-1

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.