banner68
banner58

Straika hatari Asante Kotoko kutua Msimbazi

Aliisumbua sana ngome ya Simba chini ya Pascal Wawa, kocha Simba ataka asajiliwe

Straika hatari Asante Kotoko kutua Msimbazi

Aliisumbua sana ngome ya Simba chini ya Pascal Wawa, kocha Simba ataka asajiliwe

11 August 2018 Saturday 07:56
Straika hatari Asante Kotoko kutua Msimbazi

Simba hii acha kabisa, ni kama utani vile lakini taarifa ikufikie tu kuwa Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amefunguka kuvutiwa zaidi na rasta wa Asante Kotoko, Yacouba Songne, imeelezwa.

Aussems ameeleza kuwa straika huyo ni balaa tupu na akisema kama isingekuwa dirisha dogo basi angefanya mazungumzo na mabosi wake ili kumsajili straika huyo hatari.

Mapema mara baada ya mchezo wa kirafiki kati ya Simba na Kotoko kumalizika pale Uwanja wa Taifa, Agosti 8, Mbelgiji huyo alifunguka na kueleza hakuna Kocha ambaye anaweza akaacha kumsajili mchezaji wa aina kama ile.

Katika mechi hiyo, Songne aliupiga mwingi mno na kuwapa tabu zaidi mabeki wa Simba ikiwemo Pascal Wawa na Erasto Nyoni.

Hata hivyo amesema ayafanya mchakato wa kuzungumza na waajiri wake ikiwezekana katika dirisha dogo aweze kusajiliwa na timu hiyo ambayo kwa sasa ina jeuri na fedha za mwekezaji wake, Mohammed Dewji Mo.

Wakati Mbelgiji huyo akifunguka juu ya Songne, Simba ipo mjini Ruangwa hivi sasa na leo inashuka dimbani kukipiga na Namungo FC kwa ajili ya mchezo wa kirafiki na uzinduzi wa Uwanja wa Majaliwa.

Updated: 11.08.2018 08:01
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
juventus 2018-09-04 11:31:37

Tunawaomba Mabosiwa Simba Kumsajili Uyo Straika Wa Kotoko Jamani 2zidikutisha Sana SIMBA NGUVU MOJA