Swedi Mkwabi ajiuzulu uenyekiti Simba SC

Swedi Mkwabi ajiuzulu uenyekiti Simba SC

14 September 2019 Saturday 23:06
Swedi Mkwabi ajiuzulu uenyekiti Simba SC

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam.

MWENYEKITI wa klabu ya Simba SC, Swedi Mkwabi amejiuzulu nafasi yake hiyo.

Taarifa ya Simba SC inaeleza :

Uongozi wa klabu ya Simba unatoa taarifa kwa wanachama, mashabiki na wananchi wote kwamba Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Swedi Mkwabi kwa uamuzi wake mwenyewe amejiuzulu nafasi ya Uenyekiti.

Katika barua ambayo Swedi ameiandikia Bodi ya Wakurugenzi kupitia Mwenyekiti wa Bodi amesema sababu kuu ya kijiuzulu nafasi hiyo ni kuhitaji muda zaidi kusimamia shughuli zake binafsi.

Bodi ya Wakurugenzi na Sekretarieti ya Simba inamtakia kila la heri katika shughuli zake, na tunatumaini kwamba ataendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali za klabu kama ilivyokuwa awali kabla kupata nafasi hiyo.

Utaratibu wa kumpata Mwenyekiti mpya tutawatangazia hapo baadae

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.