Tamasha la uchangiaji wa Elimu Kiba na Samatta, Makonda na Wizara ya Elimu ndani

Tamasha hilo litafanyika kila mwaka na katika mikoa mbalimbali

Tamasha la uchangiaji wa Elimu Kiba na Samatta, Makonda na Wizara ya Elimu ndani

Tamasha hilo litafanyika kila mwaka na katika mikoa mbalimbali

08 June 2018 Friday 11:48
Tamasha la uchangiaji wa Elimu Kiba na Samatta, Makonda na Wizara ya Elimu ndani

Na Amini Nyaungo

Ali Kiba amesema mfululizo wa michezo ya hisani ya uchangiaji wa Elimu wa shule za Tanzani ni wakudumu na utakuwa endelevu kila mwaka na utafanyika mara kwa mara wakibadilisha mikoa.

Amesema watafanya mara mbili kwa mwaka, huku Dar es salam na Mwanza ni sehemu pekee ambayo itanufaika na awamu hii ya kwanza.

Homa ya kuelekea pambano hilo la Juni 9, 2018 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, inazidi kupanda ambapo Ali Kiba na Mbwana Samatta kila mmoja atakuwa na timu yake ili kuwaburudisha na kuhamasisha wapenzi wa soka jijini humo kwa pamoja kutokana na umaarufu wa Ali Kiba kama mwanamuziki na Mbwana Samatta ambaye ni mchezaji nyota wa timu ya taifa na Genk ya nchini Ubelgiji ambapo kila mmoja anafanya vizuri katika kazi zake.

"Tutamfunga Samatta, kuanzia leo navaa uhusika wa bifu naye lakini kwa upande wa mchezo huo hadi siku ya mchezo wenyewe, Juni 9, 2018, na hii itakuwa endelevu kila mwaka hadi tutakapokufa," alisema Ali Kiba.

Kiba pia amegusia ukubwa wa tukio hilo huenda likafanyika na Wizara ya Elimu wakatoa neno lao kuelekea mchezo huo, huku mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwa amebariki kufanyika kwa mchezo huo.

Tamasha hilo litadhaminiwa na Maziwa ya Asas huku wakisoma watakuwa pamoja katika tamasha hilo pamoja na kushiriki kikamikifu Katika kusaidia jamii ya Watanzania.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.