Tenga asaka ubosi Fifa

Achuana na wagombea wengine kutoka mataifa kadhaa Afrika

Tenga asaka ubosi Fifa

Achuana na wagombea wengine kutoka mataifa kadhaa Afrika

11 September 2018 Tuesday 12:58
Tenga asaka ubosi Fifa

Rais wa zamani wa TFF na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Leodegar Tenga amepitishwa na kamati ya maadili ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), kuwania nafasi ya mjumbe wa Baraza la Shirikisho hilo akiwakilisha kundi la nchi za Afrika zinazozungumza lugha ya Kiingereza.

Nafasi hiyo ni ile iliyoachwa wazi na Rais wa Shirikisho la Soka la Ghana (GFA), Kwesi Nyantakyi aliyefungiwa na FIFA.

Jumla ya viongozi watano wa mpira wa miguu kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wamepitishwa kuwania nafasi hiyo sambamba na Tenga.

Ukimuondoa Tenga ambaye pia ni Mjumbe wa kamati ya utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), wagombea wengine ni Danny Jordaan (Afrika Kusini), Nick Mwenda (Kenya), Elvis Chetty (Shelisheli) na Walter Nyamilandu (Malawi).

Katika mchujo huo uliompitisha Tenga, Rais wa Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), Moses Magogo na Adam Methethwa wa Swaziland walienguliwa kuwania nafasi hiyo.

Uchaguzi wa kumpata mshindi wa nafasi hiyo linatarajiwa kufanyika jijini Cairo, Septemba 28.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.