Tetesi za soka Ulaya Agosti 1, 2019

Tetesi za soka Ulaya Agosti 1, 2019

01 August 2019 Thursday 06:38
Tetesi za soka Ulaya Agosti 1, 2019

Manchester United wako tayari kukabiliana na Barcelona katika kumpata mshambuliaji wa klabu ya Marseille mwenye umri wa miaka 17 Mfaransa Isaac  Lihadji msimu huu. (La Provence, via Mail)

Nia ya Aston Villa ya kumsaka mshambuliaji wa Brentford Mfaransa Neal Maupay imeongezeka zaidi baada ya Sheffield United kupunguza kasi ya kumuania  . (Birmingham Mail)

Sunderland watamruhusu kiungo wao  na nahodha George Honeyman, mwenye umri wa miaka 24, kujiunga na kikosi cha Hull City . (Northern Echo)

Manchester United bado hawajaamua kuhusu suala la kumchukua Paulo Dybala, huku mshambuliaji huyo wa Argentina , 25, akitarajia kujadili na Juventus juu ya hali yake ya baadae wiki hii . (Manchester Evening News)

Dybala ameiambia klabu ya United kuwa itatakiwa kumpa mkataba wenye thamani ya pauni 350,000 kila wiki ikiwa atajiunga nao. (Mail)

Rais wa klabu ya Lille Gerard Lopez amethibitisha kuwa winga wa Ivory Coast Nicolas Pepe mwenye umri wa miaka 24 atauzwa kwa Arsenal kwa euro milioni 80. (RMC Sport - in French)

Napoli wamejipanga kwa dau la Euro milioni 60 kwa ajili ya winga wa Crystal Palace na mchezaji wa kimataifa wa Ivory Coast Wilfried Zaha baada ya kumkosa Pepe. (Mail)

Arsenal wamejiandaa kumuacha mlinzi wao Mjerumani Shkodran Mustafi aondoke msimu huu, lakini Roma bado hawajaweka dau kwa ajili yake licha ya kwamba wanahusishwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27.(Romanews, via Star)

Juventus amethibitisha kumewepo kwa  ofa kwa ajili ya mshambuliaji wake raia wa Argentina Paulo Dybala, huku  Manchester United na Tottenham wanaongoza katika kumuwania . (Mirror)

Mlinzi wa zamani wa Barcelona Carles Puyol, mwenye umri wa miaka 41, amesema kuwa alikataa mara mbili ombi la Real Madrid la kutaka ajiunge nao. (AS in Spanish)

Meneja wa Rangers Steven Gerrard amethibitisha kuwa uhamisho wa winga wa Liverpool Muingereza Ryan Kent, ambaye ana umri wa miaka 22, haupo na kwamba hawawezi kumudu uhamisho wake wa kudumu . (Daily Record)

Zenit St Petersburg wanatarajia kutangaza kusaini mkataba na winga wa Barcelona Malcolm, mwenye umri wa miaka 22,baada ya klabu mbili  hizo kukubaliana kuhusu garama zake . (Goal)

Barcelona wanataka kumuuza Mbrazili Philippe Coutinho, lakini hawajapata ofa yoyote kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 . (ESPN)

Arsenal itakuwa na deni  kufuatia kumsajili kwa mkopo mlinzi wa Juventus na Italia Daniele Rugani mwenye umri wa miaka 25 kwa ajili ya kuwa naye kwa misimu miwili. (Gazzetta dello Sport, via Sun)

Nahodha Laurent Koscielny, mwenye umri wa miaka 33, bado ameazimia kuondoka Arsenal msimu huu licha ya mazungumzo yanayoendelea baina yake na klabu hiyo.(Independent)

Updated: 03.08.2019 07:31
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.