Tetesi za soka Ulaya Agosti 11, 2019

Tetesi za soka Ulaya Agosti 11, 2019

11 August 2019 Sunday 07:09
Tetesi za soka Ulaya Agosti 11, 2019

Jose Mourinho amekuwa mchambuzi wa masuala ya soka wa kituo cha Sky Sports na leo Jumapili ataanza uchambuzi katika mechi kati ya  Manchester United and Chelsea. (Sky Sports)

Juventus hawajakata tamaa ya kumsajili kiungo wa Man United, Mfaransa  Paul Pogba, 26. (Express)

Pamoja na kuwepo taarifa za kuhama, Pogba amesisitiza kuwa hatowavuruga(kuwasumbua) wachezaji wenzake katika chumba cha kubadilishia nguo klabuni hapo. (Mirror)

Bayern Munich wapo katika hatua ya mwisho ya kukamilisha usajili wa kiungo Mcrotia Ivan Perisic, 30, kutoka klabu ya Inter Milan kwa mkopo na kwamba baadae itamsajili kwa ada ya paundi milioni 23.5. (Sky Italia via Sky Sports)

Ofa ya Manchester United ya paundi milioni 24 ya kumnunua kiungo wa klabu ya Dinamo Zagreb, Muhispania Dani Olmo  21 ilikataliwa kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili la Uingereza Alhamisi wiki hii. (Sportske Novosti via Mirror)

Meneja wa zamani wa Everton na Manchester United, David Moyes yupo  katika orodha ya makocha wanaotarajiwa kufundisha  klabu ya Inter Miami inayomilikiwa na  David Beckham's. (Mirror)

Mshambuliaji wa Juventus, Muargentina  Paulo Dybala, 25, amesafiri na klabu yake hiyo kucheza mechi ya mwisho ya kirafiki ya kujipima nguvu  dhidi ya Atletico Madrid jijini Stockholm. Anahusishwa kuhamia klabu ya Paris St-Germain.(Mail)

Juventus wamekasirishwa na mchezaji wao kiungo, Sami Khedira,32, baada ya mjerumani huyo kakataa ofa mbalimbali ikiwemo kutoka klabu ya Wolves na Asernal. (Calciomercato via Sun)

Klabu ya Celtic, Besiktas na Rennes bado wanagombea saini ya winga wa Everton  Yannick Bolasie, 30, ambaye pia amekataa ofa ya klabu ya Urusi ya CSKA Moscow. (Goal)

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.