Tetesi za soka Ulaya Agosti 14, 2019

Tetesi za soka Ulaya Agosti 14, 2019

14 August 2019 Wednesday 06:44
Tetesi za soka Ulaya Agosti 14, 2019

WAWAKILISHI wa klabu ya Paris St-Germain na Barcelona wamekutana rasmi kwa saa tatu kujadili dili la uhamisho la mshambuliaji, Neymar(27). Hata hivyo bado hawajafikia muafaka wa suala hilo. (Le Parisien - in French)

Barca wanajiandaa kuwapa PSG paundi milioni 93 mshambuliaji, Philippe Coutinho, 27, na kiungo Mcroatia Ivan Rakitic, 31, ili kumpata Neymar. (ESPN)

PSG wameitaka Barca katika ofa hiyo pia wamuongeze na beki wa kulia Mreno Nelson Semedo, 25, na kwamba wataridhika. (Mail)

Manchester United sasa wapo tayari kupokea ofa yoyote nzuri ya kumuuza kiungo wake Mfaransa Paul Pogba, 26, kabla ya dirisha la usajili Ulaya kufungwa (Telegraph)

Man United wapo tayari kulipa sehemu ya mshahara wa Alexis Sanchez(30) endapo Mchile huyo atakubali kujiunga kwa mkopo katika klabu ya Roma ya Italia(Sun)

Kwa sasa nafasi ya Sanchez, Man United inathibitiwa ipasavyo na mshambuliaji kinda Mason Greenwood (17) baada ya kufanya vizuri katika mechi za maandalizi na ya ufunguzi wa ligi ya EPL.Sanchez alikuwa majeruhi. (Sun)

Beki Mbelgiji wa klabu ya Tottenham Toby Alderweireld, 30, yupo tayari kuvunja mkataba wake wa mwaka mmoja uliosalia klabuni hapo ili dirisha la usajili lijalo aondoke kama mcheza huru. (Mirror)

Beki Mcroatia Dejan Lovren, 30, hakufanya mazoezi na timu yake ya Liverpool kujiandaa na fainali ya UEFA Super Cup dhidi ya Chelsea hii leo. Hii ni kufuatia kuwepo kwa mazungumzo ya kuhamia klabu ya Roma ya Italia. (Telegraph)

Newcastle United wapo katika mazungumzo ya kumuongezea mkataba mpya kiungo wao Sean Longstaff, 21, ambaye anahusishwa na kujiunga na Manchester United. (Times)

Klabu ya Flamengo ya Brazil ipo katika mazungumzo na klabu ya Marseille ili kumsajili mshambuliaji Mario Balotelli(29) kwa mkataba wa miaka miwili. (Corriere dello Sport - in Italian)

Klabu ya MLS DC United inataka kumsajili mshambuliaji Muingereza Daniel Sturridge(29) ambaye yupo huru baada ya msimu uliopita kuitumikia klabu ya Liverpool. (ESPN)

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.