Tetesi za soka Ulaya Agosti 15, 2019

Tetesi za soka Ulaya Agosti 15, 2019

15 August 2019 Thursday 06:49
Tetesi za soka Ulaya Agosti 15, 2019

Alexis Sanchez amekataa kuondoka Man United katika kipindi hiki cha usajili na bosi wake Ole Gunnar Solskjaer amemtishia kumuwela benchi. Mchezaji huyo anawindwa na klabu ya Roma. (Sun)

Vilevile klabu ya AC Milan, Juventus na Napoli nao wanamwinda Mchile huyo mwenye miaka 30. (Mail)

Real Madrid imekataa ombi la Paris St-Germain kumjumuisha Vinicius Junior, 19, katika dili la uhamisho la mshambuliaji wa Kibrazil Neymar, 27. (AS)

Pia tetesi zinaeleza , PSG wanataka katika dili hilo kiungo Mcroatia Luka Modric, 33, na kiungo Mbrazil Casemiro, 27, wajumuishwe . (Marca)

Neymar ameendelea kufanya mazoezi binafsi akisubilia kukamilika kwa dili la uhamisho wake. (Esporte Interactivo, via Mundo Deportivo - in Spanish)

Kiungo mshambuliaji wa Kibrazil Philippe Coutinho, 27, anatarajiwa kujiunga na PSG na hato jumuishwa katika mpango wa dili la Neymar. (Goal)

Manchester United wanatarajia kumuongezea mkataba mpya beki wake raia wa Sweden, Victor Lindelof, 25, Ataongezewa paundi 75,000 ya mshahara wake wa kila wiki. (Aftonbladet - in Swedish)

Bayern Munich wamerejea tena katika kuwania saini ya winga wa Manchester City, Mjerumani Leroy Sane ambaye atakuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi saba akiunguza majeraha yake. (Bild - in German)

Mshambuliaji wa Marseille, Muitalia Mario Balotelli, 29, amekataa ofa ya kujiunga na klabu ya Brazil ya Flamengo. Sasa anajiandaa kujiunga na klabu ya Brescia kwa mkataba wa miaka mitatu (Guardian)

Flamengo wanaamini watamshawishi Baloteli kujiunga na klabu hiyo na sasa wanamtumia kaka wa mshambuliaji huyo Enock amshawishi. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Winga wa Everton,Mnaigeria Alex Iwobi, 23, amesema ameondoka Asernal ili kulinda kipaji chake. (Mirror)

Tottenham wapo katika mazungumzo ya kumbakisha klabuni hapo kiungo Christian Eriksen, 27, kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili la Ulaya Septemba 2. Mdenmark huyo anawindwa na Juventus, Real Madrid. (Independent)

Updated: 15.08.2019 06:53
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.