Tetesi za soka Ulaya Agosti 16, 2019

Tetesi za soka Ulaya Agosti 16, 2019

16 August 2019 Friday 04:52
Tetesi za soka Ulaya Agosti 16, 2019

KLABU ya Flamengo ya Brazil inaamini itampata na imetenga paundi milioni 4 ili kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Marseille Mario Balotelli,29, Japo mwenyewe anataka kujiunga na klabu ya Brescia . (Mail)

Kiungo wa Man United, Mfaransa Paul Pogba bado anataka kuihama klabu hiyo ajiunge na Real Madrid katika kipindi hiki cha dirisha la usajili. (Marca)

Beki wa kati wa Uingereza Harry Maguire(26) alikataa ofa ya mshahara wa paundi 278,000 kwa wiki kutoka Man City ili ajiunge na Man United. (Star)

Meneja wa Man United, Ole Gunnar Solskjaer amefanya mazungumzo na kiungo wa Tottenham, Mdenmark Christian Eriksen, 27, ili ajiunge na klabu hiyo japo mchezaji huyo anataka kuelekea nchini Hispania (Manchester Evening News)

Mshambuliaji wa Man United, Mchile Alexis Sanchez, 30, anajiandaa kujiunga na mojawapo ya vilabu hivi, Juventus, Napoli, AC Milan na Inter Milan (Mirror)

Sanchez anatarajiwa kuondoka klabuni hapo kabla ya dirisha la usajili barani Ulaya kufungwa Septemba 2. (Times)

Mshahara wa Sanchez wa paundi 560,000 kwa wiki ndio unailazimu kwa sasa Man United kumuuza mchezaji huyo. (Mirror)

Juventus bado wanaamini kuwa watamuuza mshambuliaji wao, Muargentina Paulo Dybala, 25, kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Independent)

Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Paris St-Germain Leonardo amesema mshambualiji wao Mbrazil Neymar "amefanya makosa". (RMC - in French)

Golikipa wa Stoke City na Uingereza Jack Butland, 26, anataka kuondoka klabuni hapo ili kutengeneza mazingira mazuri ya kuitwa tena katika timu ya taifa itakayoshiriki mashindano ya Yuro 2020. (Mail)Napoli ilikataa ofa ya paundi milioni 82 kutoka Man United ili kumsajili beki, Msenegali Kalidou Koulibaly(28) kabla ya dirisha la usajili la Uingereza kufungwa (Corriere dello Sport, via Calciomercato)

Winga wa Bournemouth, Muingereza Jordon Ibe,23, anawindwa na klabu ya Celtic. Pia Napoli nao wanawania saini yake. (Sun)

Meneja wa West Ham, Manuel Pellegrini anataka kipa wa Liverpool Adrian,32, abakie klabuni hapo. (Mail)

Napoli imekubali dili la kumsajili winga wa PSV Eindhoven,Mmexico Hirving Lozano(23). (Voetbal International - in Dutch)

Updated: 16.08.2019 05:02
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.