Tetesi za soka Ulaya Agosti 17, 2019

Tetesi za soka Ulaya Agosti 17, 2019

17 August 2019 Saturday 10:13
Tetesi za soka Ulaya Agosti 17, 2019

MENEJA wa Arsenal Unai Emery amesema hakutegemea kama usajili waliofanya katika dirisha la usajili lingeimarisha kikosi chake. (Mirror)

Kocha wa timu ya taifa ya Brazil, Tite amesema hatma ya mshambuliaji Neymar, 27, ipo kwa klabu ya Paris St-Germain. (Marca)

Kiungo wa Tottenham, Moussa Sissoko amesema kuwa alilia sana mara baada ya kushindwa kuchukua ubingwa wa klabu bingwa Ulaya(UEFA). Walifungwa na Liverpool.(Talksport)

Kiungo wa Liverpool, Xherdan Shaqiri, 27, anatafakari kuhusu hatma ya kuendelea kuwepo katika klabu hiyo endapo atakuwa apangwi mara kwa mara katika mechi. (Langenthaler Tagblatt via Daily Star)

Beki wa zamani wa Liverpool Jamie Carragher amesema Tottenham itaathirika sana endapo itampoteza mshambuliaji wake Harry Kane, 26, lakini si kwa kiungo Christian Eriksen, 27, anayetaka kuondoka klabuni hapo. (Daily Telegraph)

Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane anafurahia uwepo wake kikosi kiungo mshambuliaji James Rodriguez, 28,.Mcolombia huyo anatajwa kuondoka klabuni hapo(Corriere dello Sport - in Italian)

Endapo beki wa kulia, Andrea Conti ,25, ataihama klabu ya AC Milan, nayo itaakikisha inamsajili beki wa kulia wa Tottenham, Muivory Coast Serge Aurier, 26 kuzuiba pengo hilo (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Kaka wa Paul Pogba,26, Mathias amesema mchezaji huyo anataka kuondoka Man United ili ajiunge na Real Madrid.(El Chiringuito via Daily Mail)

Mshambuliaji wa Edin Dzeko, 33,ameongeza mkataba wa miaka mitatu kuitumikia klabu yake ya AS Roma. Alihusishwa kujiunga na Inter Milan. (AS Roma)

Winga Muholanzi Steven Bergwijn, 21,ameingia mkataba wa miaka mitano na klabu ya PSV Eidhoven. Alikuwa akiwindwa na Man United na Bayern Munich. (Goal)

Updated: 17.08.2019 10:17
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.