Tetesi za soka Ulaya Agosti 2, 2019

Tetesi za soka Ulaya Agosti 2, 2019

02 August 2019 Friday 06:40
Tetesi za soka Ulaya Agosti 2, 2019

Liverpool wanataka  kumnunua mshambuliaji wa Bordeaux na Guinea Francois Kamano na wako tayari kutoa  paundi milioni 20 kwa mchezaji  huyo  mwenye umri wa miaka 23 . (Sun)

Manchester City wamekataa dau la paundi milioni 72 kutoka kwa Bayern Munich kumsajili mshambuliaji Leroy Sane raia wa Ujerumani, mwenye umri wa miaka 23. (Metro)

City wanataka walipwe pauni milioni 137 kwa mauzo ya Sane ikiwa hatakuwa na haja ya kusaini mkataba wa kurefusha mkataba wake, unaomalizika Juni 2021. (Telegraph)

Manchester United wanapambana kufikia makubaliano na mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, mwenye umri wa miaka 25, na muwakilishi wake, na hivyo kuuweka hatarini mkataba na Juventus wa kubadilishana mchezaji wa safu ya mashambulizi Mbelgiji Romelu Lukaku, mwenye umri wa miaka 26. (Independent)

Tottenham wanaufatilia mkataba wa kiungo wa kati wa Sporting Lisbon na Ureno Bruno Fernandes, mwenye umri wa miaka 24, wanataka kumsajili kama kiungo mbadala endapo wakimkosa mchezaji wa Real Beti -Giovani Lo Celso, mwenye umri wa miaka 23. (Evening Standard)

Betis wamekataa ofa kadhaa kutoka kwa Tottenham kwa ajili ya mchezaji wa kimataifa wa Argentina Lo Celso. (SevillaABC - in Spanish)

Kiungo wa kati- nyuma wa Argentina Nicolas Otamendi, mwenye umri wa miaka 31, anataka kuendelea kuwepo Manchester City licha ya kuhusishwa na taarifa za kuihama klabu hiyo.(Sun)

Manchester City imeingia tena katika mazungumzo na Juventus juu ya kiungo mkabaji Mremo Joao Cancelo, mwenye umri wa miaka 25. (Telegraph)

Mlizi wa England Harry Maguire, mwenye umri wa miaka 26, ameachwa nje ya kikosi cha Leicester kitakachocheza mechi ya kirafiki dhidi ya  Atalanta Ijumaa kutokana na hali ya sintohfahamu juu ya hali ya yake ya baadae na Foxes wanataka mkataba wa paundi milioni 90 ikiwa Manchester United watataka kupata saini yake. (Telegraph)

Dau la sasa la Manchester United kwa ajili ya Maguire ni la thamani ya paundi milioni 80 na klabu hiyo inaweza kutumia zaidi ya paundi milioni 150 kwa ujumla kabla ya kipindi cha mwisho cha mchakato wa uhamisho kukamilika (Independent)

Manchester United ilikataa fursa ya kusaini mkataba na mshambuliaji wa Juventus mwenye umri wa miaka 19 Moise Kean, na kumruhusu mtaliano huyo kuwa huru kuhamia Everton. (90min)

Newcastle wanakaribia kusaini mkataba na winga wa Ufaransa Allan Saint-Maximin,mwenye umri wa miaka 22, kutoka Nice katika mkataba wa pauni milioni 16.5 . (Talksport)

Beki wa kushoto wa Brazil, Dani Alves anakaribia kuhamia Sao Paulo. Atajiunga kama  mchezaji huru baada ya kuondoka Paris St-Germain. (Goal)

Crystal Palace wamefanya mawasiliano na Cardiff City kuhusu kiungo wa kati wa Real Betis Muhispania Victor Camarasa mwenye umri wa miaka 25

Updated: 02.08.2019 06:45
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.