Tetesi za soka Ulaya Agosti 3, 2019

Tetesi za soka Ulaya Agosti 3, 2019

03 August 2019 Saturday 07:15
Tetesi za soka Ulaya Agosti 3, 2019

KIUNGO wa kati wa Chelsea,Mfaransa N'Golo Kante,28, anasisitiza kuwa msimu huu atabakia  Stamford Bridg, licha ya taarifa zinazomuhusisha na kujiunga na klabu ya Paris St-Germain. (Express)

Kiungo wa Ureno Bruno Fernandes, anayehusishwa na taarifa za kuhamia Tottenham na Manchester United, ameliambia gazeti la Sporting Lisbon  anataka kuondoka kwenye klabu hiyo msimu huu. Sporting wanataka kulipwa  yeuro milioni 70 sawa na  paundi  milioni 64 kwa ajili yauhamisho wa  nahodha huyo mwenye umri wa miaka 24 . (Record, via Mirror)

Inasemekana Manchester United tayari wamesaini   mkataba na Fernandes baada ya kombe la Super Cup la Portugal . (Express)

Mlinzi wa zamani wa Liverpool Andrea Dossena,37, ambaye kwa sasa yuko na Piacenza, amemtaka mchezaji mwenzake katika timu ya Juventus Paul Dybala, ni bora ahamie Anfield kuliko Manchester United. (Liverpool Echo)

Tottenham wanataka mchezaji mbadala iwapo watamuuza Christian Eriksen,27, baada ya muda wa mwisho wa kipindi cha uhamisho kwa wachezajii nchini Uingereza kukamilika Alhamisi ijayo. Klabu za Hispania zina hadi Agosti 31 kusajili  wachezaji(London Evening Standard) 

Pamoja na Fernandes, Spurs wanafanya mazungumzo na Real Betis kwa ajili ya mchezaji wa kimataifa wa Argentina, Giovani lo Celso, mwenye umri wa miaka 23. (London Evening Standard)

Arsenal wanatarajia kutoa ofa mpya kwa ajili ya kiungo wa kati- wa Celtic Kieran Tierney katika siku zijazo, baada ya kukataliwa dau mara mbili za awali kwa ajili ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uskochi mwenye umri wa miaka 22 . (Sky Sports)

Hatimaye Tottenham wako tayari kukamilisha usajili wa paundi milioni 30  kumsajili beki wa kushoto Ryan Sessegnon mwenye umri wa miaka 19,  kutoka klabu  ya Fulham. (Mail)

Kiungo wa kati wa Ajax, Donny van de Beek, mwenye umri wa miaka 22, amethibitisha kuwa Real Madrid wameonyesha nia ya kumsajili. (Goal)

Klabu ya Hull watapata faida ya paundi milioni 9.45 kutokana na mauzo ya mlinzi wake wa zamani Harry Maguire kutoka kwa Manchester City. 
The Tigers walikubali mkataba wa 15% juu ya faida ya uhamisho walipomuuza kijana huyo mwenye umri wa miaka 26 kwa Leicester in 2017. (Hull Daily Mail)

Manchester City wamekataa dau la pauni milioni 72 kutoka kwa Bayern Munich kwa ajili ya mshambuliaji wa Leroy Sane raia wa Ujerumani, mwenye umri wa miaka 23. (Metro)

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.