Tetesi za soka Ulaya Agosti 4, 2019

Tetesi za soka Ulaya Agosti 4, 2019

04 August 2019 Sunday 07:59
Tetesi za soka Ulaya Agosti 4, 2019

Manchester United  wameweka mezani paundi milioni 46 kumsajili  mshambuliaji wa Ajax, Mbrazil David Neres. (Yahoo - in Portuguese)

Arsenal wapo katika mazungumzo na Barcelona ya kumsajili kwa mkopo mshambuliaji Mbrazil Philippe Coutinho, 27. Gunners watatoa paundi milioni 27 kukamilisha dili hilo. (Sun)

Kiungo wa kimataifa wa Ufaransa na Man United Paul Pobga ameingia hofu ya kutosajiliwa na Real Madrid kufuatia klabu hiyo kutakiwa kutumia paundi milioni 270 ili kufanikisha usajili wake (Mirror)

Bayern Munich wamekamilisha mazungumzo binafsi na winga wa Man City, Mjerumani Leroy Sane  23. (Sky Sport Germany - in German)

Endapo Sane ataendelea na msimamo wake wa kukataa kusaini mkataba mpya na Man City atapoteza malipo ya paundi milioni 11 . (Mirror)

Bosi wa Manchester City, Pep Guardiola anataka  kumsajili kiungo wa Real Madrid, Muhispania Isco, 27,  pia anamuhitaji beki wa klabu ya Bournemouth Nathan Ake, 24. (Express)

Bosi wa Crystal Palace Roy Hodgson anataka kumsajili beki  Muingereza,  Gary Cahill, 33 kwa mkataba wa miaka miwili. (Sun)

Barcelona wanajianda rasmi kuanza mazungumzo ya klabu ya  Paris St-Germain  ili kumrejesha mshambuliaji wa Kibrazil Neymar  27, . (Goal.com)

Kiungo  Bruno Fernandes, 24, anayehusishwa kujiunga na Man United, ameiambia klabu yake ya Sporting Lisbon anataka kujiunga  Tottenham. (Mail) 

Real Madrid imeshakubaliana na kiungo Mholanzi Donny van de Beek,22, na sasa wanasubiri makubaliano na klabu yake ya  Ajax. (Marca)

Bosi wa Leicester Brendan Rodgers anatarajia kumnunua kwa paundi milioni 15 beki wa Celtic, Mnorway, Kristoffer Ajer, 21. (Star)

Barcelona wamekubaliana na Real Betis kumsajili beki Muhispania Junior Firpo(22) kwa ada ya paundi milioni  22. (ESPN)

Burnley wanapambana Crystal Palace kuwania saini ya kiungo wa Real Betis Victor Camarasa, 25, ambaye msimu uliopita alicheza kwa mkopo akiwa na  Cardiff City. (Sky Sports)

Tottenham wanajiandaa kumsajili kiungo mwenye umri wa miaka 19 anayechezea Uingereza chini ya miaka 21 Ryan Sessegnon, kutoka Fulham, hii ni kutokana na kutokuwa na uhakika wa kumsajili  kiungo wa Real Betis, Muargentina Giovani Lo Celso. (Star)

Vilevile Spurs wapo katika mpambano na Atletico Madrid kuwania saini ya beki wa Borussia Monchengladbach, Mjerumani  Matthias Ginter, 25 ambaye yupo sokoni kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 60(Bild, via ..90min)

Pia Tottenham wapo katika mpambano na Roma na Juventus kuwania saini ya beki wa kulia wa Napoli, Mualbanian  Elseid Hysaj, 25, ambaye pia aliwania na  Chelsea . (Express)

Bosi wa Newcastle Steve Bruce anatarajia kumlazimisha mmiliki wa klabu hiyo, Mike Ashley kufanya usajili kabla ya dirisha kufungwa Alhamisi ijayo na chaguo lake la  kwanza ni kumbakisha klabuni hapo  Dwight Gayle,28, wa klabu ya Leeds. (Newcastle Chronicle)

Leicester wanamuania beki wa  Getafe, Mtogo  Djene Dakonam, 27, kama mbadala wa beki Harry Maguire anayetarajia kujiunga na Man United. (Leicester Mercury)

Chelsea imewaweka sokoni  kiungo wao Mfaransa Tiemoue Bakayoko, 24, na Muingereza  Danny Drinkwater, 29. (Telegraph)

Drinkwater anahitajika na klabu ya Brighton kwa mkopo . (Mail)

Beki wa kushoto wa Celtic Mscotland Kieran Tierney, 22, atakuwa nje kwa wiki nane kufuatia kupata majeraha. Uenda Asernal wakasitisha mpango wao wa kumwania beki huyo ambayo ilimwekea paundi milioni 25 kumsajili. (Sun)

Newcastle wapo katika mazungumzo na  Inter Milan kwa ajili ya kumsajili kwa mkopo mshambuliaji, Muargentina Facundo Colidio,19, (Mail)

Beki wa New York Red Bulls, Muamerika Aaron Long, 26, anamatumaini kuwa atapata kibali ili kujiunga na klabu ya West Ham kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Sky Sports)

Mshambualiaji wa Manchester City, Mjerumani  Lukas Nmecha, 20, anatumia misimu wa 2019-20  kwa mkopo kuichezea klabu ya  Wolfsburg. (Manchester Evening News)

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.