Tetesi za soka Ulaya Agosti 5, 2019

Tetesi za soka Ulaya Agosti 5, 2019

05 August 2019 Monday 08:24
Tetesi za soka Ulaya Agosti 5, 2019

NAHODHA wa zamani wa Uingereza Wayne Rooney, 33, anataka kurejea Manchester United kama kocha mara baada ya kustaafu kandanda. (Sun)

Rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu amegusia kuwa mabingwa hao wa Hispania huenda wakafanya usajili mwingine baada ya kuthibitisha kumsajili  Junior Firpo, 22, kutoka Real Betis. (Sport)

Inter Milan imemwambia mshambuliaji wa Argentina, Mauro Icardi, 26, kuwa hatocheza kwa miaka miwili ikiwa ataendelea kusisitiza kubakia katika klabu hiyo hadi mkataba wake utakapokamilika. (Gazzetta Dello Sport)

Barcelona imefutilia mbali uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wao wa zamani Neymar, 27, kutoka Paris St-Germain katika dirisha hili la usajili. (Goal.com)

Real Madrid wameamua kumsajili beki wa kati wa Ajax, Mholanzi Donny van de Beek, 22, badala ya kung'ang'ania usajili wa Mfaransa Paul Pogba, 26 kutoka Manchester United. (Marca)

Leicester inatathmini uwezekano wa kumsajili  beki wa James Tarkowski, 26, wa Burnley ama Nathan Ake, 24, wa Bournemouth kuchukua nafasi ya beki wao Muingereza Harry Maguire, 26, ambaye anahusishwa na harakati za kuhamia Man United. (Sky Sports)

Manchester United wameafikiana kwa mkataba wa usajili wa mwaka mmoja wenye thamani ya paundi milioni 6.2 na mshambuliaji wa Juventus Mario Mandzukic, 33 ili dili hilo kukamilika itatumika paundi milioni 15 au kuwa sehemu ya mabadilishano na Mbelgiji Romelu Lukaku(26). (Mail)

Mabingwa Manchester City wanajiandaa kukamilisha usajili wa paundi milioni 32 wa beki wa Ureno Joao Cancelo, 25, huku beki wa pembeni Mbrazil Danilo, 28, akitarajiwa kuondoka. (Mail)

Watford wamekataa dau la paundi milioni 32 kutoka kwa Everton kumnunua kiungo wa kati wa miaka 26 Mfaransa Abdoulaye Doucoure. (RMC, via Express)

Mshambuliaji wa Brentford, Mfaransa Neal Maupay 22, anatarajiwa kujiunga na Brighton kwa kandarasi ya miaka minne. (L'Equipe - in French)

Brighton inatarajiwa kukamilisha usajili wa Maupay kwa fedha za juu katika rekodi ya klabu hiyo. (Talksport)

Tottenham wanatalajia kumjumuisha Josh Onomah, 22, katika mkataba wao wa paundi milioni 30 kumsaini mlinzi wa Fulham Ryan Sessegnon, 19. (Mail)

Crystal Palace wanajiandaa kumsajili kiungo wa kati wa Hispania mwenye miaka 25- Victor Camarasa - ambaye msimu uliopita alikuwa Cardiff kwa mkopo. (Independent)
West Ham wanapania kumsajili mchezaji wa tano kabla ya dirisha la usajili kufungwa lakini hawana mpango wa kumsaini mlinzi wa zamani wa Chelsea na kiungo wa kimataifa wa England Gary Cahill, 33. (Football.London)

Updated: 05.08.2019 08:32
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.