Tetesi za soka Ulaya Agosti 6, 2019

Tetesi za soka Ulaya Agosti 6, 2019

06 August 2019 Tuesday 07:27
Tetesi za soka Ulaya Agosti 6, 2019


Manchester United wanakaribia kumsajili kiungo wa Tottenham raia wa Denmark Christian Eriksen, 27, baada ya kiungo wa Sporting Lisbon Mreno Bruno Fernandes - ambaye alikuwa anawindwa na Man United kuweka wazi nia yake ya kujiunga na Spurs. (AS)

Tottenham inaendelea kupokea ofa kutoka klabu za Ulaya kwa ajili ya Eriksen endapo mchezaji huyo hatauzwa ndani ya Uingereza mpaka dirisha litakapofungwa siku ya Alhamisi. (Telegraph)

Everton wametenga paundi milioni 100 kumsajili msahambuliaji wa Crystal Palace Wilfried Zaha, 26. Ofa hiyo inahusisha pia Everton kuwapa Palace mshambuliajii Cenk Tosun na kiungo James McCarthy, wote wana miaka 28. (Sun)

Zaha ambaye ni raia wa Ivory Coast anatarajiwa kujiunga na Everton kabla ya Alhamisi ambapo dirisha la usajili Uingereza linafungwa, Palace wapo tayari kupokea kitita cha kufikia paundi milioni 65. (Independent)

Arsenal wanaweza kuelekeza nguvu zao zote katika kumsajili beki wa kati wa RB Leipzig Mfaransa Dayot Upamecano, 20, kama mbadala wa beki wa Juventus Daniele Rugani - lakini Leipzig wanataka paundi milioni 50 ili kumuachia beki huyo. (Mirror)
Leicester haitamsajili Nathan Ake katika dirisha hili la usajili baada ya klabu ya Bournemouth kutaka dau la paundi milioni 75 kwa beki huyo raia wa Uholanzai. (Sky Sports)
Manchester United wataendelea kupokea ofa kwa ajili ya mshambuliaji wao Romelu Lukaku, 26, lakini yawezekana wasitafute mbadala wake endapo ataondoka baada ya kuchipukia kwa kinda Mason Greenwood, 17. (ESPN)

Lukaku ana uwezekano mkubwa wa kujiunga Inter Milan kuliko Juventus hususani endapo Man United itashindwa kumpata Paulo Dybala, 25. (Express)

Arsenal wamejaribu kufikia makubaliano na nahodha wao Laurent Koscielny - lakini beki huyo mwenye miaka 33, ambaye aligoma kusafiri na timu kwenda Marekani, pia amegoma kufanya mazungumzo na klabu. (Mirror)

Juventus wanajiandaa kuwapa Manchester United wachezaji watatu ili kubadilishana na kiungo Paul Pogba. (Mirror)

Mpango huo kama utafaulu, utawahusisha wachezaji Danilo, 28, na Joao Cancelo, 25. (Goal.com)

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.