Tetesi za soka Ulaya Agosti 7, 2019

Tetesi za soka Ulaya Agosti 7, 2019

07 August 2019 Wednesday 07:29
Tetesi za soka Ulaya Agosti 7, 2019


KLABU ya Crystal Palace imekataa ofa ya paundi milioni 70 kutoka kwa Everton kumnunua mshambuliaji wa Ivory Coast, Wilfried Zaha, 26.(Sun)

Everton ilikuwa imewajumuisha wachezaji kama vile mshambuliaji wa Uturuki Cenk Tosun, 28, na kiungo wa kati wa Jamhuri ya Ireland James McCarthy, 28, katika ofa hiyo. (Mail)

Tottenham wamefikia makubaliano na Juventus kuhusu uhamisho wa mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 25, kwa dau la karibu paundi milioni 62. (Sky Sports Italia, via Daily Mail)

Dybala anajiandaa kuanza mazungumzo ya mkataba na Tottenham kabla ya Alhamisi ambao ni muda wa mwisho uliowekwa kwa uhamisho wa wachezaji kukamilika. (Goal)

Tottenham pia wamedhamiria kumsaini mshambuliaji wa Barcelona Mbrazil Philippe Coutinho. (ESPN)

DC United wanajiandaa kufanya mazungumzo na wawakilishi wa kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil, 30, wanapojaribu kujaza pengo lililoachwa wazi na Wayne Rooney anayeelekea Derby. (Mirror)
Manchester United wameongeza juhudi ya kufikia mkataba na  kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen, 27. (Telegraph)

Eriksen hayuko katika mpango wa  muda mrefu wa Mauricio Pochettino(Mirror)

Uamuzi wa dakika za mwisho wa United kumhusu Eriksen unakuja licha ya tetesi ikiwa kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 26, ataendelea kuwa katika klabu hiyo hadi mwisho wa dirisha la uhamisho litakapofungwa. (Standard)

United pia wanawatarajiwa kufanya uamuzi ambao haukutarajiwa kumnyakua mshambuliaji wa zamani wa Tottenham Fernando Llorente, ambaye kwa sasa yuko huru kuondoka klabu hiyo bila malipo. (Sky Sports Italy, via Metro)

Manchester City wanatarajiwa kuthibitisha usajili wa Joao Cancelo kutoka Juventus siku ya Jumatano baada ya beki huyo wa miaka 25 raia wa Ureno kufanyiwa vipimo vya afya. (Star)

Liverpool hawana mpango wa kumuuza kiungo wa kati wa Brazil Fabinho, licha ya tetesi zinazomhusisha mchezaji huyo wa miaka 25 na uhamisho wa Real Madrid. (Echo)

Crystal Palace wanakaribia  kumsajili McCarthy kutoka Everton kwa hadi  paundi milioni 8.5. (Sky Sports)

Paris St-Germain imetoa ofa ya kumnunua mchezaji nyota wa Brazil Neymar, 27, kwa vilabu vya Manchester United, Juventus na Real Madrid.

Vilabu hivyo vinafanya kila juhudi kuhakikisha Barcelona haimsajili tena mchezaji wao wa zamani. (Sport)

Lukaku kwa mara nyingine amefanya mazoezi  na wachezaji wa chini ya miaka 18 wa Anderlecht siku ya Jumanne, bila idhini ya United kuwa mjini Brussels. (Mail)

Mshambuliaji wa Manchester United raia wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 26, hajarejea kutoka Carrington kujiunga na mazoezi ya kikosi cha kwanza licha ya tetesi zinazohusiana na hatma yake ya baadae  katika klabu hiyo. (Mirror)
Manchester United na Manchester City wametuma wataalamu wao kufuatilia kiungo wa kati wa Norway Hakon Evjen ,19 wakati wa mchuano wa Bodo/Glimt. (TV2 via Manchester Evening News)

Everton wanakaribia kumsaini kwa mkopo beki wa Monaco Mfaransa Djibril Sidibe, 27. (Mail)

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.