Tetesi za soka Ulaya Agosti 8, 2019

Tetesi za soka Ulaya Agosti 8, 2019

08 August 2019 Thursday 07:23
Tetesi za soka Ulaya Agosti 8, 2019

MSHAMBULIAJI Robert Lewandowski ametoa wito kwa Bayern Munich kuwasajili wachezaji watatu wapya. Staa huyo wa Poland anataka kuimarishwa kwa safu ya mashambulizi baada ya wachezaji nyota kuhama klabu hiyo. (Goal)

Real MAtletico Madrid wanajiandaa kumsajili kiungo  kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, 27. (Independent)

Kingo wa kati wa Juventus Sami Khedira, 32, amekataa uwezekano wa uhamisho mara mbili kwa  kuwa anataka kujiunga na Arsenal. (Star)

adrid imeanza mazungumzo na Paris Saint-Germain kuhusu mpango wa kumsajili mshambuliaji nyota wa Brazil Neymar, 27. (Sky Sports)

Azma ya Barcelona kumsajili tena Neymar, 27, inategemea ikiwa klabu hiyo itamuuza Philippe Coutinho ambaye pia ni mchezaji mwenzake wa kimataifa wa Brazil. (Goal)

Manchester United wako tayari kulipa paundi milioni 81 kumnyakua mshambuliaji wa Hispania na Athletic Bilbao Inaki Williams, 25. (El Chiringuito TV - via Mail)

Pendekezo la Leroy Sane kuhamia Bayern Munich kutoka Manchester City limeathiriwa na jeraha la goti linalomkabili nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani. (Mail)
Beki wa Chelsea Mbrazil David Luiz, 32, ataruhusiwa kujiunga na Arsenal kwa  paundi milioni 8 tu. (Mirror)

Mshambuliaji wa Crystal Palace Wilfried Zaha,26, amewasilisha ombi la kutaka uhamisho huku kukiwa na tetesi kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast akipigiwa chapuo kuhamia Everton. (Express)

Palace wameiambia Everton hawatakubali kupokea chini paundi milioni100 kumwachilia mshambuliaji Zaha. (Guardian)
Everton wanatarajia kumsajili beki wa Chelsea na kiungo wa kimataifa wa England wa wachezaji wa chini ya miaka 21 Fikayo Tomori, 21, na beki wa kati wa Bournemouth Mholanzi Nathan Ake, 24. (Sun)

Newcastle wanakaribia kumsajili beki wa kulia, Emil Krafth, 25, kutoka klabu ya Ufaransa ya Amiens. (Newcastle Chronicle)

Burnley wamewasilisha ombi la dakika ya mwisho kumsaini kiungo wa kati, Danny Drinkwater, 29, kwa mkopo kutoka Chelsea. (Mail)
Tottenham wanakaribia pia kumsaini beki wa kushoto wa Fulham Ryan Sessegnon, 19. (Mirror)

Wolves wamesitisha mpango wa kumsajili kiungo wa kati wa Southampton na Gabon Mario Lemina, 25. (Express & Star - via Daily Echo)

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.