Tetesi za soka Ulaya Julai 10, 2019

Tetesi za soka Ulaya Julai 10, 2019

10 July 2019 Wednesday 05:16
Tetesi za soka Ulaya Julai 10, 2019

Asernal wanataka kumsajili bila malipo yoyote ya ada ya usajili mshambuliaji  wa klabu ya Marseille, Muitaliano Mario Balotelli, 28, (Mirror)

Barcelona wanataka kumsajili kiungo mshambuliaji, Mromania Romania Ianis Hagi, ambaye ni mtoto wa zamani wa mchezaji wa klabu hiyo Georghe Hagi, kutoka klabu ya Real Valadolid. (AS - in Spanish)

Bilionea wa Kiingereza anataka kuinunua klabu ya Nice ya nchini Ufaransa (L'Equipe - in French

Barcelona sasa ipo katika harakati za kuitaka saini ya beki wa Man united, Mswiden, Victor Lindelof, 24,  hii ni baada ya beki Mholanzi  wa klabu ya Ajax Matthijs de Ligt kutaka kujiunga na  Juventus. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Real Madrid wanataka kuweka rekodi ya dunia ya usajili kwa kutoa paundi milioni 162 ili kumsajili kiungo wa Man United, Mfaransa, Paul Pogba(26)  (Marca)

Meneja wa klabu ya Sheffield Wednesday  Steve Bruce anatarajia kujiunga na  Newcastle kurithi mikoba iliyoachwa wazi na Rafael Benitez. (Chronicle)

Kocha msaidizi wa Manchester City, Mikel Arteta na kocha wa  timu ya  Nice,  Patrick Vieira  wamekataa ofa ya kuwa kocha  mpya wa  Newcastle  kuziba nafasi iliyoachwa na Benitez. (Sun)

Everton ni miongoni mwa timu zinazowania saini ya kiungo wa  Manchester City, Muingereza, Fabian Delph, 29. (Sky Sports)

Meneja wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer anataka mshambuliaji wake, Mbelgiji
 Romelu Lukaku, 26, kuachana na mpango wake wa kuamia klabu ya  Inter Milan na abaki Old Trafford. (Sun)

Arsenal wametoa ofa ya paundi milioni 18 kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid, Mariano Diaz, 25. (Star)

Everton wanampango wa kumsajili mshambuliaji wa mwenye umri wa miaka 19 Muitaliano, Moise Kean kutoka klabu  ya Juventus inayotaka ilipwe paundi milioni 31. (Mail)
Klabu ya Fenerbahce inataka  kumchukua kwa kwa mkopo kiungo wa Asernal, Mjerumani Mesut Ozil (Sky Sports)

Manchester United wamewasiliana na  Southampton  kuangalia uwezekano wa kumsajili kiungo wa klabu hiyo, Mgaboni Mario Lemina 25 (  Sky sports)

Bournemouth wamempa mkataba wa miaka mitano mshambuliaji wake, Muingereza,Callum Wilson (27). Mchezaji huyo alikuwa akiwaniwa  na West Ham, Chelsea na Everton. (Sun)

Liverpool wanaamini mshambuliaji wake, Mbelgiji,Divock Origi, 24, atasaini mkataba mpya wa kubaiki klabuni hapo. (ESPN)

Crystal Palace watamsajili moja kwa moja msgambuliaji wa Swansea, Mghana Jordan Ayew, 27, ambaye msimu uliopita aliichezea klabu hiyo kwa mkopo. (Sky Sports)

Mpango wa West Ham kumsajili mshambuliaji wa Celta Vigo, Muuruguay axi Gomez   (22)umevunjika   baada ya kushindwa kuafikiana makubaliano mshahara wake (Sky Sports)

Updated: 10.07.2019 06:24
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.