Tetesi za soka Ulaya Julai 11, 2019

Tetesi za soka Ulaya Julai 11, 2019

11 July 2019 Thursday 04:53
Tetesi za soka Ulaya Julai 11, 2019

BEKI wa kati wa Chelsea David Luiz anaamini kurejea kwa  Frank Lampard kama mkufunzi wa klabu hiyo kutarejesha ari na utamaduni wa soka wa klabu hiyo. (Standard)

Arsenal wanataka kumsajili winga wa Barcelona Mbrazil , Malcom, 22,  huku Everton ikiwa imeshaweka mezani dau la paundi milioni 31.5 kupata saini ya Mbrazil huyo. (Sun)

Mshambualiji  wa zamani wa  Liverpool Dean Saunders anaamini kuwa  mkufunzi wa sasa wa Man United Ole Gunnar Solskjaer hawezi kupata mafanikio klabuni hapo (talkSPORT) 

Solskjaer anamatumaini kuwa atafanikiwa kuipiku Man City katika kupata saini ya beki wa kati, wa Leicester City, Muingereza Harry Maguire(26). Sasa Man United imekubali kutoa paundi milioni 75   (Mail)

Kiungo wa Manchester United, Muhispania , Juan Mata, 31, amekataa ofa ya kuliipwa mshahara paundi 550,000 kila wiki kutoka klabu ya  Shanghai  ya China na sasa anataka kusaini mkataba mpya na Man United. (90Min)

Mata amesema ataka kubakia klabuni hapo kwa  kuwa yupo katika  moja ya klabu nne  bora duniani (MUTV)

Wiki iliyopita kocha  Sam Allardyce alikataa ofa ya kuwa mkufunzi wa Newcastle United . (Mail)

Roma wanamtaka beki wa Tottenham, Mbelgiji  Toby Alderweireld 30.  Wametenga paundi milioni 25 kumnyakua kabla ya Julai 26. (Sky Sports)

Everton wameonesha nia ya kumsajili mshambualiji wa Lille, Muivory Coast Nicolas Pepe. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 atawagharimu paundi milioni 58.5 ili kumpata. (Telegraph)

Kiungo wa Southampton (25) Mario Lemina, ambaye ananyatiwa na vilabu yya Manchester United, Arsenal and Leicester, amesema msimu ujao hataki kuichezea klabu hiyo. (France Football, via Daily Echo)

Tottenham wameongeza nguvu ili kupata saini ya kiungo wa  Real Madrid, Dani Ceballos, 22, kwa mkopo (Mirror)

Arsenal wapo tayari kumtoa beki wake, Calum Chambers, 24, Carl Jenkinson, 27, au kiungo wake Mohamed Elneny, 26, kama sehemu ya kumpata winga wa  Crystal Palace, Wilfried Zaha. Tayari Gunners wameshaweka mezani ofa ya  paundi milioni 40 kumnyaka winga hiyo mwenye umri wa miaka 26 ambayo imekataliwa na Palace(Mirror)

Manchester City wanataka kumbakisha kiungo wao, Fabian Delph japo kuna tetesi kuwa  mchezaji huyo mwenye miaka 29 anataka kuondoka klabuni hapo. (Metro)

Mchezaji wa timu ya taifa ya Uingereza china ya miaka 21, Ezri Konsa, amefanya vipimo vya afya katika klabu ya Aston Villa kabla ya kuiacha klabu yake ya Brentford. (Sun)

Wolves na  West Ham  ni miongoni mwa vilabu
vinavyowania saini ya beki, Mmexico Edson Alvarez (21) anayekipiga  katika ligi ya Marekani  akichezea timu ya  Liga MX. (Marca Claro, via Sport Witness)

Aston Villa, Brighton, Bournemouth na Wolves wanapigana vikumbo kuinasa saini ya winga wa Liverpool, Harry Wilson, 22, ambaye msimu ulioisha aliichezea Derby Country kwa mkopo. (Birmingham Mail)

West Brom wamekanusha taarifa kuwa beki wake, Ahmed Hegazi, 28,anataka kujiunga na klabu ya Al -Ahli ya  ya nchini Saudi Arabia. (Birmingham Mail)

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.