Tetesi za soka Ulaya Julai 12, 2019

Tetesi za soka Ulaya Julai 12, 2019

12 July 2019 Friday 04:57
Tetesi za soka Ulaya Julai 12, 2019

Manchester United wapo katika mazungumzo na klabu ya Roma ya Italia ya kumuuza mshambuliaji wake Mbelgiji Romelu Lukaku|(26). (Goal.com)

Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Inter Milan, Piero Ausilio amesafiri kuelekea Ungereza kwa lengo la kukutana na  Manchester United ili kufanikisha mpango wa kumsajili mshambuliaji wa klabu hiyo, Lukaku. (Guardian)

Wakala wa beki wa Tottenham, Mbelgiji Toby Alderweireld anafanya mazungumzo na klabu ya Roma ili imsajili mchezaji huyo kwa ada ya  paundi kati ya milioni 22.5 hadi 25. (Calciomercato)

Barcelona wanatarajia kukamilisha mpango wake wa kupata saini ya mshambuliaji Mfaransa, Antoine Griezmann(28) kutoka klabu ya  Atletico Madrid baada ya kukubali kulipa ada ya uhamisho ya paundi milioni 107. (Mirror)

Mshambuliaji Gareth Bale, 29, ameanza mazoezi na timu yake ya Real Madrid iliyoweka kambi nchini Canada na anajitahidi kuwepo katika mipango ya kocha Zinedine Zidane. (Mail)

Klabu ya Newcastle inamtaka mkufunzi wa sasa wa klabu ya  Sheffield Wednesday, Steve Bruce akakinoe kikosi hicho msimu ujao na inatumai atakwenda nacho nchini China kwa maandalizi ya msimu wa ligi  (Telegraph)

Imetenga paundi milioni 5 kama fidia ya kuvunja mkataba wa kumkoa kocha huyo . (Times)

Manchester United na Manchester City wanagombea kupata saini ya kiungo wa klabu ya Sporting Lisbon, Bruno Fernandes mwenye umri wa miaka 24 (Mirror)

Mshambuliaji wa Real Madrid, Mariano Diaz, 25, kwa sasa hayupo tayari kujinga na klabu ya  Arsenal  (AS, via Mirror)

Paris St-Germain inajiandaa kupeleka ofa nzuri kwa klabu   ya Everton ili kumnyakua  kiungo, Msenegal  Idrissa Gueye(29). Inataka kutoa paundi milioni 27. (L'Equipe, via Sun)

Arsenal wanapambana kupata saini ya kiungo wa Real Madrid, Mhispania Dani Ceballos(22)  kwa mkopo. Tayari kiungo huyo yupo katika mazungumzo na klabu ya   Tottenham. (Sky Sports)

Mkufunzi wa Liverpool, Jurgen Klopp anataka kumzuia, kocha wa Rangers Steven Gerrard asimrejeshe klabuni kwake, winga  Ryan Kent(22) ambaye yupo Liverpool kwa mkopo . (Express)

Wakala wa winga wa  PSV Eindhoven, Steven Bergwijn, 21, ameimbia Bayern Munich taarifa za kwamba mchezaji wake huyo anataka kujiunga na Man United ni za uongo. (Express)

Manchester United imepuuzilia mbali taarifa kwamba inampango wa kutaka kumsajili kiungo wa klabu ya  Southampton, Mgabon Mario Lemina, 25, ambaye pia anahusishwa na kuamia  Arsenal. (Manchester Evening News)

Mshambuliaji wa Bournemouth, Muingereza  Callum Wilson, 27  aliyekuwa akiwindwa na klabu ya  West Ham, ameongeza mkataba wa miaka minne na klabu yake hiyo. (Talksport)

Bournemouth wapo tayari kumuachia bila ada yoyote ya  usajili winga wake, Mskotishi  Ryan Fraser(25) ambaye anahusishwa na kujiunga na klabu  ya Arsenal, katika dirisha dogo la usajili na si kwa sasa.(Express)

Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza, Peter Crouch, 38, ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Burnley atatoa maamuzi ya kustaafu soka au la mara tu baada ya mkataba wake kumalizika  klabuni hapo. (Talksport)

Newcastle anamnyatia mshambuliaji, Mbrazil Joelinton Hoffenheim 22, ambaye pia anawaniwa na  klabu ya  Wolves. (Newcastle Chronicle)

Winga wa Crystal Palace,  Muivory Coast, Wilfried Zaha ambaye anatakiwa na  Arsenal, hayupo katika mipango ya klabu yake hiyo . (Express)

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.