Tetesi za soka Ulaya Julai 13, 2019

Tetesi za soka Ulaya Julai 13, 2019

13 July 2019 Saturday 07:20
Tetesi za soka Ulaya Julai 13, 2019

KLABU ya Juventus imekubali kulipa dau la paundi milioni 63 kumnunua beki wa Ajax, Mholanzi Matthijs de Ligt mwenye umri wa miaka 19. (De Telegraaf - in Dutch)

West Ham wanataka kulipa kitita cha paundi milioni 10 ili kumsajili kiungo wa kati wa Equatorial Guinea Pedro Obiang, 27, licha ya klabu za Itali kama vile Bologna na Sassuolo kuonyesha hamu ya kumnunua mchezaji huyo. (Sun)

West Ham ipo katika mazungumzo na klabu ya Eintracht Frankfurt ili kumsani mshambuliaji wa timu hiyo, Mfaransa Sebastian Haller(25) kwa ada ya paundi milioni  40. (Sky Sports)

Tottenham inatarajia kuwasilisha ombi la kumsajili kiungo wa kati wa Leeds, Muingereza Kalvin Phillips, ambaye klabu hiyo ya York Shire inasema ana thamani ya  paundi milioni 30. (Mirror)

Manchester United bado ipo katika mpambano wa kuwania saini ya kiungo wa kati wa Newcastle, Muingreza Sean Longstaff kutoka Newcastle licha ya klabu hiyo kutokubaliana juu thamani ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Sky Sports)

Lakini bei ya Newcastle ya  paundi milioni 50 inaweza kuifanya United kujitoa katika mpambano huo (ESPN)

Manchester United wameongeza dau la paundi milioni 30  ya thamani ya kiungo wake, Mfaransa Paul Pogba, 26, na sasa wanataka dau la paundi milioni 180 kumuuza mchezaji huyo waliyemnunua kwa dau la paundi milioni 89 mwaka  2016 kutoka Juventus.(Star)

Juventus wamesitisha hamu yao ya kutaka kumsajili Pogba, wakitoa fursa kwa Real Madrid kumsaini mchezaji huyo wa Ufaransa. (Mail)

Manchester United huenda ikamsajili beki wa Monaco na Ufaransa 19 Benoit Badiashile,ambaye pia anawaniwa na Wolves - iwapo watamkosa beki wa Leicester City, Muingereza Harry Maguire, 26. (L'Equipe, via Express)

Inter Milan huenda wakalazimika kulipa takriban paundi milioni 90 ili kumsajili mshambuliaji wa Ubelgiji na Man United Romelu Lukaku, 26, msimu huu (Telegraph)

Arsenal inataka kulipwa dau la paundi milioni 8.8 ili kumuuza nahodha wake, beki  Mfaransa Laurent Koscielny, 33 ambaye anataka kuondoka katika klabu hiyo na ambaye alikataa kuungana na wenzake kuelekea Marekani kwa mechi za maandilizi ya msimu ujao. (London Evening Standard)

Arsenal imeongeza nguvu ya kupata saini ya beki wa Benfica, Mreno Ruben Dias, 22, hiyo ni kutokana na  maamuzi ya hivi karibuni ya Koscielny (Mail)

Updated: 15.07.2019 05:05
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.