Tetesi za soka Ulaya Julai 14, 2019

Tetesi za soka Ulaya Julai 14, 2019

14 July 2019 Sunday 07:33
Tetesi za soka Ulaya Julai 14, 2019

Kiungo wa Everton, Msenegal Idrissa Gueye(29) anajua uwepo wa tetesi za yeye kujiunga na klabu ya Paris St-Germain lakini anasema kwa sasa akili yake ipo katika mashindano ya Afcon 2019. (Sport Witness)

Kiungo wa Barcelona, Mbrazil  Philippe Coutinho(27) anatarajia kukataa ofa ya kujiunga Manchester United  na pia hataki kurejea klabu yake ya zamani  Liverpool na sasa anataka kujiunga na klabu ya  Paris St-Germain.(Express)

Hata hivyo Barcelona  wamemuahakikishia Coutinho kubaki klabuni hapo lakini wakala wake anashinikiza aondoke katika klabu hiyo (Sky Sports)

Bayern Munich  bado hawajakata tamaa ya kuwania saini ya mshambuliaji wa Chelsea, Muingereza Callum Hudson-Odoi(18) na inatarajia wiki hii kuweka ofa ya kumsajili ya paundi milioni 45 . (Mail)

Manchester United imesema ifikapo Agosti 8, na Real Madrid ikishindwa kutoa kiwango inachokitaka haitomuuza kiungo wake, Mfaransa Paul Pogba . (Mirror)

Beki wa Leicester, Muingereza  Harry Maguire, 26 anaitaka klabu yake hiyo kukubali ofa ya Man United ya paundi milioni 75 ili ajiunge na mashetani wekundi wa Old Traford (Mail)

Pia mchezaji huyo anailalamikia klabu yake hiyo ya Leicester City kuongeza dau la usajili wake kwa vilabu vya Man United na Man City la hadi paundi milioni 70 ambalo awali lilikataliwa na klabu hizo. (Sun)

Kiungo mchezeshaji wa timu ya Tottenham, Mdenmark  Christian Eriksen(27) anataondoka katika klabu hiyo. (Guardian)

Liverpool imeingia katika mpambano wa kumwania mshambuliaji wa CSKA Moscow, Fedor Chalov   kwa 
kutoa ofa ya paundi milioni 20. Mchezaji huo mwenye umri wa miaka 21 pia anawindwa na klabu ya Arsenal, Manchester City, Tottenham, Chelsea na  Man United (Mirror)

Tottenham bado wanaendelea na mpango wao kwa kuinyaka saini ya kiungo wa Real Betis, Muargentina Giovani lo Celso(23). Pia inamtaka kiungo wa Lyona ya Ufaransa Nabil  Fekir, 25. (Football.London)

Arsenal wamerudi kwa mara ya pili wakiwa na ofa ya paundi milioni 25 ili kumsajili beki wa Celtic, Mscotland Kieran Tierney (22)baadaya ofa yao ya kwanza ya paundi milioni 15 kukataliwa na klabu ya Celtic mwezi Juni. (Mail)

Arsenal wameingia katika mpambano wa kuipata  saini ya kiungo wa Roma, Muitali Nicolo Zaniolo(20). Klabu ya Tottenham na Juventus nazo zinamwania mchezaji huyo (Calciomercato)

Licha ya bosi wa chama cha soka cha Senegal, Saer Seck kudai moja ya klabu kubwa nchini Hispania imemuwekea ofa kubwa mshambuliaji Sadio Mane, Klabu yake ya sasa Liverpool imekanusha taarifa hizo  na kwamba haijafanya mazungumzo yoyote na klabu ikiwemo Real Madrid. (Liverpool Echo)

Klabu ya Napoli na Atletico Madrid wapo katika mazungumzo ya mwisho ya usajili wa beki Mualbania  Elseid Hysaj,25, anayehusishwa na kujiunga na Manchester United. (Football Italia)

Kiungo wa Dinamo Zagreb, Muispania Dani Olmo(21) anamatuamini ya kujiunga na klabu ya Man United. (Manchester Evening News)

Updated: 15.07.2019 06:25
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.