Tetesi za soka Ulaya Julai 15, 2019

Tetesi za soka Ulaya Julai 15, 2019

15 July 2019 Monday 04:57
Tetesi za soka Ulaya Julai 15, 2019

Manchester United imekubali kulipa ada ya usajili ya paundi milioni 80 kumsajili beki wa Leicester, Muingereza Harry Maguire(26) ambaye anaweka historia ya kuwa beki ghali zaidi duniani. Leo Jumatatu atafanyiwa vipimo vya afya. (Sun)

Leicester wanatarajia kuziba nafasi hiyo kwa kumsajili beki wa Brighton, Muingereza Lewis Dunk(27), ambaye watalipa ada ya paundi milioni 45. (Sun)

Celtic wameikataa ofa ya Asernal ya paundi milioni 25 ya usajili wa beki wa kushoto, Mskotishi Kieran Tierney(22) (Sky Sports)

Manchester City wanaamini winga wao, Mjerumani Leroy Sane(23) ataikataa ofa ya Bayern Munich na kubakia klabuni hapo. (Daily Mirror)

Tottenham na Arsenal wameingia kwenye anga za Man City kumgombea  beki wa Kibrazil, Dani Alaves (36) ambaye ni mchezaji huru akitokea klabu ya  Paris St-Germain ya nchini Ufaransa. (Mundo Deportivo via Daily Mail)

Rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu amesema Atletico Madrid hawana ushahidi wowote wa kwamba klabu hiyo ilianza mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji, Mfaransa Antonie Griezman(28) tangu mwezi Machi mwaka huu. (Goal)

Arsenal inamwania mshambuliaji wa Everton, Mbrazil, Gremio (23) . (Mirror)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema klabu yake itajaza nafasi ya beki wake wa kushoto majira ya kiangazi wakati ambapo beki wake wa sasa, Mskotish  Andrew Robertson, 25, ataondoka. (ESPN)

Wiki hii Liverpool wanatarajia kumchukua kwa   mkopo  kiungo wa klabu ya Doncaster, Muingereza  Herbie Kane(20) ambaye pia anawaniwa na klabu ya  Brentford, Charlton  na Hull City. (Goal)

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.