Tetesi za soka Ulaya Julai 16, 2019

Tetesi za soka Ulaya Julai 16, 2019

16 July 2019 Tuesday 05:55
Tetesi za soka Ulaya Julai 16, 2019

KOCHA wa zamani wa Manchester United, Jose Mourinho anatarajiwa kujiunga na moja ya kilabu nchini Ujerumani. (Independent)

Leicester wameahidi kumuuza beki wake, Muingereza Harry Maguire, 26, endapo Manchester United au Manchester City wataongeza dau zaidi ili kuvunja rekodi ya  paundi milioni 75 iliyowekwa na Liverpool kumnunua beki wake,  Virgil van Dijk. (Telegraph)

Mchezaji wa Paris St-Germain, Mbrazil  Neymar, 27, atakutana kwa mazungumzo na mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Leonardo kujadili mustakabali wake. (ESPN)

Newcastle  italazimika kulipa paundi milioni  4 kwa klabu ya  Sheffield Wednesday ili kumnyaka kocha  Steve Bruce. (Sun)

Bruce  anatarajia kuondoka na wasaidizi wake Steve Agnew na Stephen Clemence kujiunga   St James' Park. (Newcastle Chronicle)

Ndani ya wiki tatu Manchester United watawasilisha ofa kwa klabu ya Sporting Lisbon ya kumsajili kiungo, Mreno  Bruno Fernandes, 24, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa  Ole Gunnar Solskjaer kukisuka upya kikosi chake. (Independent)

Mkurugenzi wa klabu ya Roma, Gianluca Petrachi amethibitisha nia ya klabu hiyo ya kutaka kumsajili beki wa  Tottenham, Mbelgiji  Toby Alderweireld, 30. (Football Italia)

Alderweireld  na  Tottenham wamemshawishi kiungo mchezeshaji wa klabu hiyo,Mdenmark Christian Eriksen 27  kuondoka na timu hiyo kwenda nchini Singapore  siku ya Jumatano japo kiungo huyo anataka kuondoka klabuni hapo (London Evening Standard)

Kiungo wa Barcelona, Mbrazil Philippe Coutinho, 27, uenda akarejea katika klabu yake ya zamani ya Liverpool kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 88. (Calciomercato, via Sport Bible)

Bayern Munich bado hawajakata tamaa ya kumsajili winga wa Man City, Mjerumani Leroy Sane, 23, wanatarajia kuweka mezani ofa ya paundi milioni 100. (Sky Germany, via Mail)

Arsenal bado wapo katika mazungumzo na klabu ya Celtic ya kumsajili beki wa kushoto, Mskotish Kieran Tierney(22) baada ya ofa yao ya pili ya paundi milioni 25 kukataliwa. (London Evening Standard)

Klabu ya Inter Milan imekubali kulipa kwa awamu ada ya uhamisho ya paundi milioni 75 ya mshambuliaji wa Man United  Romelu Lukaku, 26. Inter wamependekeza kulipa kwa miaka miwili yaani paundi milioni 9, kisha paundi milioni 27 kisha paundi milioni 27 lakini Man United wanataka walipwe fedha yote. (Star)

Mshambuliaji wa West Brom, Mvenezuela  Salomon Rondon atajiunga na kocha wake wa zamani Rafael Benitez  ambaye sasa ni mkufunzi wa klabu ya China ya  Dalian Yifang. (Express and Star)

West Ham wapo katika mazungumzo na ya kumsajili mshambuliaji wa   Eintracht Frankfurt, Mfaransa Sebastien Haller, 25. (London Evening Standard)

Arsenal imemtuma daktari  nchini Brazil kwa ajili ya kumpima vipimo vya afya mshambuliaji wa Everton, Mbrazil Gremio, 23. (Fox Sports, via Calciomercato)

Winga wa zamani wa  Arsenal, Marc Overmars, ambaye kwa sasa ni mkurugenzi mkuu wa klabu ya Ajax, ameshauri wamsajili winga Mmorocco Hakim Ziyech(26) kwa paundi milioni 22 awe mbadala wa kiungo mchezeshaji, Mjerumani Mesut Ozil. (Calciomercato)

Vile vile Overmars amesema wapo katika hatua za mwisho za kukamilisha kumuuza beki wa klabu ya Ajax, Mholanzi Matthijs de Ligt 19 kwenda klabu ya Juventus. (Goal.com)

Barcelona nao pia wamewasilisha ofa yao ya kutaka kumsajili beki hiyo wa kati, De Ligt. (Mundo Deportivo)

Wolves wanamnyatia kwa karibu  beki wa Lazio, Mbrazil Wallace, 24. (Birmingham Mail)

Galatasaray wanapambana na AC Milan kuwania saini ya kiungo wa Fulham, Jean Michael Seri, 27. (Fanatik, via Sport Witness)

Kiungo Mzimbabwe Marvelous Nakamba, 25, amekataa kujiunga katika mazoezi na timu yake Club Brugge akishinikiza auzwe kwenda Aston Villa. (Birmingham Mail)

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.