Tetesi za soka Ulaya Julai 18, 2019

Tetesi za soka Ulaya Julai 18, 2019

18 July 2019 Thursday 05:00
Tetesi za soka Ulaya Julai 18, 2019

Ofa ya Arsenal ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Crystal Palace, Muivory Coast Wilfried Zaha 26, imeendelea kukataliwa. (Mirror)

Pep Guardiola amefungua milango ya kuondoka kwa winga wa Man City,Mjerumani  Leroy Sane, 23, anataka auzwe kwa paundi milioni 100. (Mirror)

Real Madrid imepanga kuwatoa washambuliaji Gareth Bale, 30, na  James Rodriguez, 28, kama sehemu ya kuongeza fedha za ununuzi wa kiungo wa Manchester United, Mfaransa Paul Pogba(26). (Marca, via Sun)

Hata hivyo ajenta  wa Pogba, Mino Raiola amekataa taarifa ya  kwamba kiungo huyo anataka kurejea Juventus. (AS)

Mbrazil Neymar amefungua milango kwa Man United imsajili kutoka klabu ya Paris Saint-Germain. (Mundo Deportivo, via Sun)

Mkufunzi wa sasa wa Newcastle, Steve Bruce atalazimika kutumia zaidi ya paundi milioni 90 kwa ajili ya usajili katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi. (Sky Sports)

Bruce alikuwa ni kocha wa 11 katika idadi ya makocha waliokuwa wakihitajika klabuni hapo baada ya kuondoka kwa Rafael Benites. (Daily Mail)

Klabu ya Hoffenheim wamethibitisha kuwa ipo katika mazungumzo ya mwisho na Newcastle United inayotaka kumsajili mshambuliaji, Mbrazil Joelinton, 22, ambaye anatarajiwa kuweka rekodi ya usajili klabuni hapo (Chronicle Live)

Kocha wa Leicester, Brendan Rodgers amemuonya beki wake Harry Maguire(26) ambaye atajiunga na Man United kutobweteka akiwa klabuni hapo (Independent)

Liverpool haifikirii kumuuza golikipa wake Simon Mignolet, 31, na wala hawana mpango wa kumtoa kwa mkopo kipa huyo katika kipindi hiki cha usajili. (Liverpool Echo)
Manchester United wanainyatia kwa karibu saini wa kiungo wa Roma Nicolo Zaniolo(20). (Mirror)

Mshambuliaji Romelu Lukaku, 26,  bado anania ya kutaka kujiunga na klabu ya Inter Milan. (Times - subscription required)

Mkufunzi wa timu ya Asernal, Unai Emery amesema kabla ya dirisha la usajili kufungwa na msimu wa ligi kuanza  klabu hiyo itasajili wachezaji wapya watatu hadi wanne. (Independent)

Beki Laurent Koscielny, 33, yupo katika mazingira tata baada ya kukataa kujiunga na wachezaji wenzake katika  ziara ya maandalizi ya msimu nchini Marekani. (L'Equipe) 

Kiungo wa Asernal  Granit Xhaka anatarajiwa kurithi mikoba ya unahodha kutoka kwa  Koscielny. (Telegraph)

Mashabiki na wapenzi wa klabu ya Juventus wamempa heshima ya kiistaa Mino Railo ambaye ni wakala wa beki Matthijs de Ligt (19)kwa kufanikisha dili la uhamisho la mchezaji huyo kutoka Ajax ambaye jana Jumatano amefanya vipimo vya afya. (Metro)

Arsenal wanaendelea kupambana ili kupata saini ya beki wa  Celtic, Mscotland Kieran Tierney anatarajiwa kusajiliwa kwa kitika kikubwa cha fedha japo  Gunners wanakutana na ushindani wa usajili wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (Scotsman)

Burnley wanatarajia kutoa kitita cha paundi milioni 12 kumsajili kipa Muingereza Tom Heaton 33. ambaye pia klabu ya Aston Villa imeweka mezani paundi milioni 8 ili kumnyaka. (Birmingham Mail)

Ashley Cole amekanusha tetesi za yeye kujiunga na Chelsea kuwa kama sehemu ya dawati la ufundi. Amebainisha hayo akiwa katika uwanja wa ndege akielekea Japan. (Mirror)

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.