Tetesi za soka Ulaya Julai 20, 2019

Tetesi za soka Ulaya Julai 20, 2019

20 July 2019 Saturday 07:57
Tetesi za soka Ulaya Julai 20, 2019

Everton imejitumbukiza katika mpambano na klabu ya Asernal ya kuwania saini ya mshambuliaji wa Crystal Palace, Muivory Coast, Wilfried Zaha(26) ambaye klabu yake imetangaza kumuuza kwa ada ya paundi milioni 80. (Evening Standard)

Mkufunzi wa Chelsea, Frank Lampard ameitaka klabu ya Everton kusahau suala la kumbakisha klabuni hapo beki, Mfaransa Kurt Zouma. Zouma (24)msimu uliopita aliichezea Everton kwa mkopo (Mirror) 

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester City,Edin Dzeko, 33, anatarajiwa kuihama klabu yake ya Roma ambayo kaichezea kwa miaka mitatu na sasa anataka kujiunga na  Inter Milan iliyoweka mezani ofa ya pundi milioni 13.5 kusajili mshambuliaji huyo raia wa  Bosnia. (Sportitalia)

Klabu ya Manchester United, Everton  na Paris St-Germain wanagombea kupata saini ya kiungo mshambuliaji wa Juventus, Mfaransa, Blaise Matuidi(32). (Le Parisien - in French)

Manchester United wamevunja mpango wao wa kumsajili kiungo wa Lazio, mzaliwa wa Hispania lakini mwenye uraia wa Serbia, Sergej Milinkovic-Savic. (Mirror)

Inter Milan  bado wanamtaka mshambuliaji wa  Man United, Lukaku  mbali na  fedha ya ada ya uhamisho wapo tayari kumtos na Mauro Icardi
Liverpool wanamnyatia kwa karibu  beki wa kushoto wa klabu ya Augsburg,Mjerumani  Philipp Max, 25,  ili kuongeza ushindani  kwa beki wake wa sasa wa Anfield Andy Robertson. (Sport - in Spanish)

Tottenham na West Ham wanagombea kupata saini ya beki wa Real Sociedad, Mhispania Diego Llorente(25). (El Mundo Deportivo)

Wolverhampton Wanderers wanataka kumsajili mshambuliaji wa AC Milan, Muitalia Patrick Cutrone,21, anayeuzwa kwa paundi milioni 20. (Express & Star)

Tottenham wamempa ofa ya mwaka mmoja wa kuichezea klabu hiyo, mshambuliaji Mhispania Fernando Llorente mwenye umri wa miaka 34, ambaye mshahara wake kwa wiki ilikuwa ni paundi 100,000 . (Mail) 

Crystal Palace  wameweka mezani ofa ya usajili ya paundi milioni 8 kwa kiungo wa Everton na wa timu ya taifa ya Jumhuri ya Ireland, James McCarthy(28)  (Sky Sports)

Winga wa  timu ya Brighton, Mfaransa   Anthony Knockaert, 27, anataka kuhamia klabu ya Fulham. Kwa sasa klabu hizo zipo katika makubaliano ya ada ya uhamisho(Argus)

Sheffield United wanataka   kumsajili  golikipa wa  Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza chini ya miaka 21 Dean Henderson. Kipa huyo mwenye umri wa miaka  22 ambaye yupo kwa mkopo amesaidia  klabu hiyo kurejea katika ligi kuu nchini humo msimu wa mwaka 2019/2020 (Sheffield Live)

Beki wa Chelsea, raia wa Wailes Ethan Ampadu (18) anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya tayari kujiunga na klabu ya Ujerumani ya  RB Leipzig. (Sky Sports)

Klabu ya Ubelgium ya Club Brugge inampango wa kumsajili mshambuliaji wa  Brighton, Muafrika Kusini Percy Tau (25) ambaye pia ameshiriki katika mashindano ya Afcon 2019 nchini Misri. (Argus)

Derby County wanampango wa kumchukua  kwa mkopo golikipa wa klabu ya Watford, Muaustria Daniel Bachmann (25). (Derby Telegraph)

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.