Tetesi za soka Ulaya Julai 21, 2019

Tetesi za soka Ulaya Julai 21, 2019

21 July 2019 Sunday 07:20
Tetesi za soka Ulaya Julai 21, 2019

GOLIKIPA, Muhispania David de Gea, 28, amekubali kusaini mkataba mpya wa miaka sita kuichezea klabu ya Man United. Mkataba huo utamfanya kuwa kipa anayelipwa fedha nyingi duniani. (Sunday Telegraph)

Beki wa kushoto wa Tottenham, Muingereza  Danny Rose, 29, amepata ofa ya kujiunga na  Barcelona. (Sport - in Spanish)

Vile vile klabu ya Italia ya Juventus pia inamtaka  beki huyo mzoefu. (Sunday Mirror)

Mkufunzi wa Newcastle, Steve Bruce anataka kumsajili mshambuliaji, Muingereza Andy Carroll. Mchezaji huyo mwenye miaka 30 yupo huru baada ya kumaliza mkataba wake mwezi Juni na West Ham. (Sun on Sunday)

Mshambuliaji wa Tottenham, Mholanzi  Vincent Janssen, 25, anatarajia kuhamia nchini Mexico katika klabu ya Monterrey  wiki ijayo. (Football London)

Arsenal wanampango wa kumsajili mshambuliaji wa  Juventus, Muitaliano Moise Kean, 19, tayari wameshafanya mazungumzo na wakala wake. (Mail on Sunday)

Watford wapo katika mazungumzo na klabu ya  Rennes  ya kumsajili mshambualiaji Msenegal Ismaila Sarr(21). (Sky Sports)

Aston Villa wanatarajia kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa klabu ya Kasimpasa, Mmisri Trezeguet, 24,. Imetenga paundi milioni  8.75. (Sunday Telegraph)

Crystal Palace wapo  katika mazungumzo ya kumsajili beki wa kulia wa Liverpool,Muingereza Nathaniel Clyne(28). Wanamtaka ili kuziba nafasi ya  Aaron Wan-Bissaka, aliyejiunga Manchester United . (Mail on Sunday) 

Beki wa Saint-Etienne, Mfaransa William Saliba, 18, anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya  siku ya Jumanne , tayari kujiunga na Asernal. The Gunners wametenga paundi milioni 28 kumsajili. (Sunday Mirror)

Itawagharimu Tottenham  kulipa paundi milioni 67 ili kumsajili kiungo wa  Real Betis, Muargentina Giovani lo Celso, 23,. (Evening Standard)

Sheffield United na Aston Villa wanagombea kupata saini ya mshambuliaji wa  Brentford, Mfaransa Neal Maupay(22). (Sun on Sunday)

Beki wa Celtic, Mscotiland  Kieran Tierney, 22, amefanya makubaliano binafsi kujiunga na   Arsernal . (Football Insider)
Newcastle wanataka kumsajili winga wa  Burnley, Muingereza Dwight McNeil, 19,  wamemtengea paundi milioni. (Sun on Sunday)

West Ham wametoa ofa ya kumsajili beki wa kati wa New York Red Bulls, Mmarekani Aaron Long. Mchezaji huyo mwenye miaka  26 ametengewa paundi milioni 4 za usajili wake. (Sky Sports)

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.