Tetesi za soka Ulaya julai 22, 2019

Tetesi za soka Ulaya julai 22, 2019

22 July 2019 Monday 05:06
Tetesi za soka Ulaya julai 22, 2019

Real Madrid imezipiga chini takribani ofa sita za kutaka kumsajili kiungo mchezeshaji wa timu hiyo, Muhispania Marco Asensio(23) ambaye kwa sasa anahusishwa kujiunga na klabu ya Liverpool. (Cadena SAR)

Baada ya kumkosa Leroy Sane na Gareth Bale klabu ya Bayern Munich imehamishia mawindo yake kwa winga wa Crystal Palace, Muivory Coast Zaha, 26, . (90min)

Burnley iliweka mezani paundi  milioni  11 kumsajili winga wa Barcelona, Muhispania  Marc Cucurella(20) kabla  hajajiunga  kwa mkopo na klabu  . (Marca)

Klabu ya china ya Beijing Guoan wanapambana kupata saini ya winga wa  Madrid, Gareth Bale(30). Wanataka kuweka rekodi ya kumlipa fedha nyingi katika historia ya ligi hiyo.. (Telegraph)

Sasa ni wazi Manchester United ambayo awali walitaka kumsajili   Bale, hawatomsajili tena. (Manchester Evening News)

Manchester United wamefanikiwa kutimiza masharti ya kumsajili beki wa Leicester City, Muingereza Harry Maguire. Mchezaji huyi mwenye umri wa miaka 26 atarajiwa kutua Old Trafford kwa paundi milioni 80. (Bleacher Report)

Pia Manchester City bado wapo katika mpambano huo wa kuwania saini ya Maguire lakini wanalazimika  kuwauza mabeki wake  Nicolas Otamendi, 31, na  Eliaquim Mangala, 28, ili kufanikisha dili hilo. (Mirror)

Beki wa Arsenal, Mfaransa  Laurent Koscielny, 33, amefanikisha mpango wake wa kuhamia klabu ya  Rennes ya Ufaransa. (RMC Sport)

Arsenal wanatarajia kuishinda  Tottenham kwenye usajili wa kiungo wa Real Madrid, Muhispania  Dani Ceballos. Mchezaji huyo mwenye miaka 22 anatarajia kujiunga na Asernal kwa mkopo. (Mirror)

Kiungo wa Liverpool, Muingereza James Milner, 33, bado hajawa na uhakika wa kubaki klabuni hapo japo mwenyewe anataka mkataba wa muda mrefu. (Liverpool Echo)

Crystal Palace wameweka mezani ada ya usajili ya paundi milioni 20, kumnyaka beki Muingereza Reece James ambaye kakataa kujiunga na Chelsea. Kinda huyo wa miaka 19 msimu uliopita aliicheza  Wigan kwa mkopo.(Star)

Arsenal, Chelsea, Manchester United na  West Ham wanapambana kuwania saini ya mchezaji wa  Dynamo Kiev, Myukraine Mykola Shaparenko (20) . (Caught Offside)

Updated: 22.07.2019 05:11
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.