Tetesi za soka Ulaya Julai 23, 2019

Tetesi za soka Ulaya Julai 23, 2019

23 July 2019 Tuesday 05:05
Tetesi za soka Ulaya Julai 23, 2019

Barcelona wanampango wa kuanza mazungumzo na galacha wao, Muargentina Lionel Messi, 32, ili kurefusha mkataba wa mshambuliaji huyo hadi miaka minne. (ESPN)

Atletico Madrid wamemuweka katika rada zao za usajili kiungo mchezeshaji wa Real Madrid,  Mcolombia James Rodriguez, 28, na uenda ikaachana na mpango wa kumsajili kiungo wa Tottenham, Mdenmark Christian Eriksen, 27. (Marca)

Antoine Griezmann, 28, amesema endapo usajili wake wa kutua Barcelona utavunjika, ni ngumu kujiunga na  Manchester United na angependelea kujiunga Asernal,  ili awe karibu na Mfaransa mwezake, mshambuliaji Alexandre Lacazette, 28, . (Goal.com)

Hatma ya usajili wa kiungo wa Man United, Mfaransa Paul Pogba, 26, kwenda Real Madrid inategemea hadi hapo mshambuliaji wa timu hiyo, Gareth Bale(30) atakapoondoka. (AS)

Bale, anaepokea paundi 550,000 kwa wiki anamkataba  hadi mwaka 2022. Anataka alipwe chake chote ili aondoke klabuni hapo. (Sky Sports)

Pia Bale anatalipwa bonasi ya paundi milioni 20 endapo atakubali kujiunga na moja ya klabu nchini China. (Mail)

Tottenham wanatarajia kutoa kitita cha fedha za usajili wiki hii kwa kunasa saini ya kiungo wa  Real Betis, Muargentina Giovani lo Celso, 23,. Pia klabu hiyo itamsajili beki wa Fulham, Muingereza anayechezea timu ya taifa chini ya miaka  21, Ryan Sessegnon mwenye umri wa miaka 19. (Mirror)

Fulham wanataka walipwe paundi milioni 40 kwa mchezaji huyo  lakini Spurs wanataka kutoa paundi milioni 25. Hata hivyo  kinda huyo anagombewa na klabu ya Manchester United Paris St-Germain, Juventus na Borussia . (London Evening Standard)

Beki wa Spurs, Mbelgiji Toby Alderweireld(30) anataka kubaki klabuni hapo japo mkataba wake unamaliziki Alhamisi ya wiki hii na uenda akaondoka klabuni hapo kama mchezaji huru. Klabu ya Roma ya Italia inamvizia kwa karibu beki huyo na imeweka mezani paundi milioni 25. (Telegraph)

Mkufunzi wa zamani wa Chelsea Maurizio Sarri ambaye kwa sasa ni kocha wa Juventus, anataka kumsajili beki wa Tottenham, Muingereza Danny Rose, 29,. (Mail)

Beki, Muingereza Harry Maguire, 26, bado yupo na klabu yake ya Leicester japo tetesi za kuamia kwake Man United  zinavuma kwa kishindo. (Leicester Mercury)

Kipa wa Manchester United, Muhispania  David de Gea, 28, anajiandaa kuboresha mkataba wake wa kulipwa paundi milioni 117 hadi mwaka 2025. Pia kipa huyo anataka kuwa nahodha wa timu hiyo. (Manchester Evening News)

Juventus wapo tayari kumuuza mshambuliaji wao, Muargetina Paulo Dybala, 25, kwenda Man United. Wanataka kulipwa  kati ya paundi milioni 70 hadi 90. (Mail)

West Brom wanaipigania kuinyaka saini ya winga wa  Sporting, Mreno Matheus Pereira, 23,. Klabu yake inataka ilipwe paundi milioni 9 za ada ya usajili wake. (Express and Star)

Mshambuliaji wa zamani wa Crystal Palace,  Clinton Morrison anatarajia winga wa klabu hiyo, Muivory Coast Wilfried Zaha, 26, atabaki klabuni hapo licha ya kutakiwa na klabu ya Arsenal na Bayern Munich. (Talksport)

Wolves wanajipanga kupeleka ofa ya pili kwa klabu ya Olympiacos ili kumnyaka beki Pape Abou Cisse, 23. (Sport Witness, via Birmingham Mail)

Kiungo wa Brighton, Taylor Richards, 18, amesema ni rahisi kuicha  Manchester City kuliko klabu yake hiyo  (Argus)

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.