Tetesi za soka Ulaya Julai 26, 2019

Tetesi za soka Ulaya Julai 26, 2019

26 July 2019 Friday 05:11
Tetesi za soka Ulaya Julai 26, 2019

Manchester United wanajiandaa kwa kuondoka kwa kiungo, Mfaransa Paul Pogba(26) na sasa wameongeza nguvu kumsajili kiungo wa Lazio, Mserbia Sergej Milinkovic-Savic, 24.Anauzwa kwa paundi milioni 70 (Mirror)

Hata kama, Pogba atabakia klabuni hapo kwa msimu mmoja, bado Man United itamsajili Milinkovic-Savic (Express)

Manchester United wameambiwa na Newcastle kuwa watalazimika kutumia zaidi ya paundi milioni 30 kumsajili kiungo wa klabu hiyo, Muingereza Sean Longstaff. (Manchester Evening News)

Everton wanampango wa kutoa paundi milioni 60 na mshambuliji Mturuki, Cenk Tosun(28) kwa klabu ya Crystal Palace kama sehemu ya makabaliano ya kupata saini ya winga, Muivory Coast Wilfried Zaha, 26 . (Telegraph)

Sasa Manchester United watailazimisha klabu ya Leicester City  inayotaka  kulipwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 80 ili kumuuza beki, Muingereza Harry Maguire. Hii ni kufuatia beki wa Man United,Muivorian  Eric Bailly kuumia hapo jana katika mechi ya kirafiki na Tottenham ambapo Man United ilishinda. (Mirror)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp ametupilia mbali tetesi kuwa klabu hiyo inataka kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale, 30,na kwamba anatumia muda wake kukiimarisha kikosi chake. (Independent)

Ada ya mauzo ya beki wa Spurs, Mbelgiji Toby Alderweireld(30) imeongezeka  kutoka paundi milioni 25 (Sun)

Aston Villa wanatarajia kufikisha idadi ya wachezaji 11 iliyowasajili katika msimu huu imeshatumia paundi milioni 120 na sasa intarajia kutoa paundi milioni 11 kwa klabu ya  Brugge  kumsajili kiungo Mzimbabwe  Marvelous Nakamba, 25. (Telegraph)

Mshambuliaji  wa Juventus, Mreno  Cristiano Ronaldo, 34, hatosaidia kumshawishi mshambuliaji wa  Paris St-Germain, Mbrazil  Neymar(27) kujiunga na Juventus kwa kuwa Neymar anataka kurejea  Barcelona. (Star)

Borussia Dortmund wapo katika mazungumzo ya kuwania saini ya  mshambuliaji wa Kibrazil anayekipigia kwa sasa Barcelona Malcom  kwa ada ya uhamisho ya Yuro milioni  42 sawa na paundi milioni  37.5m. (Goal)

Middlesbrough wanatarajia kupata saini ya winga, Muingereza Marcus Browne, 21,  kutoka klabu ya  West Ham United.(Teesside Gazette)

Bosi wa Napoli, Carlo Ancelotti bado yupo katika mkakati wa kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid, Mcolombia James Rodriguez, 28, . (Marca)

Wakati huo huo wakala wa winga wa  Lille, Muivory Coast, Nicolas Pepe, 24,anafanya mazungumzo na Napoli ambayo ipo tayari kumtoa kiungo wake, Mualgeria Adam Ounas, 22 pamoja na fedha zaidi ya Yuro milioni 82 (paundi milioni 73) kufanikisha mpango huo. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Mshambualiaji wa Lyon, Mfaransa Moussa Dembele  23, ni miongoni mwa wachezaji wanaotarajiwa kununuliwa na Man United endapo Romelu Lukaka(26) ataondoka klabuni hapo (Sky Sports)

Newcastle United wanakaribia kumsajili kiungo wa zamani wa Chelsea, Kyle Scott, 21, kama mchezaji huru. Mchezaji huyo amechea timu ya taifa  ya Uingereza chini miaka 16, pia ya taifa ya Ireland chini ya miaka 17 na ya Marekani chini ya miaka 18 na 20. (Newcastle Chronicle)

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.