Tetesi za soka Ulaya Julai 27, 2019

Tetesi za soka Ulaya Julai 27, 2019

27 July 2019 Saturday 07:07
Tetesi za soka Ulaya Julai 27, 2019

Atletico Madrid wanataka kumsajili kiungo wa kati, Mcolombia James Rodriguez, 28, kutoka kwa mahasimu wao Real Madrid. (Independent)

Romelu Lukaku, 26, amesafiri kwenda nyumbani Ubelgiji siku ya Ijumaa kufanya mazungumzo na wakala wake huku Inter Milan wakikaribia kufikia mkataba wa paundi milioni 70 kumnunu mshambuliaji huyo wa Manchester United. (Daily Mail)

Mshambuliaji wa Lille,Mreno Rafael Leao, 20, anajiandaa kuondoka klabuni hapo kwenda AC Milan kwa mkataba wa yeuro milioni 35 - utakaojumuisha 20% ya makataa ya kumuuza. (RMC Sport)

Real Madrid wana imani kuwa watafanikiwa kumsajili kiugo wa kati Mfaransa Paul Pogba kutoka Manchester United msimu ujao. (ESPN)

Bayern Munich wameanza mazungumzo na Manchester City kuhusu usajiliwa wa winga wao wa miaka 23 Mjerumani Leroy Sane, ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa  paundi milioni 90. (Mirror)

Mmiliki wa Newcastle Mike Ashley amesema kikubwa maishani ni "pesa kwanza kisha klabu baadae" kwa maneja wake wa zamani Rafael Benitez, na kuongeza kuwa "ni vigumu" kuendelea kumng'ang'ania raia huyo wa Uhispania. (Mail)

Bournemouth wamepania kuipiku Brighton katika usajili wa paundi milioni15 kumnunua kiungo wa kati wa Huddersfield, Philip Billing, 23. (Sun)

Swansea City wanakabiliwa na hatari ya kumkosa mchezaji wa safu ya kati wa Chelsea mwenye umri wa miaka 22-Kasey Palmer. (Wales Online)

Panathinaikos wanampango wa kumnunua kiungo wa kati wa Ivory Coast anayechezea Celtic Kouassi Eboue, 21. (Daily Record)

Beki wa Real Madrid wa miaka 22, Mhispania Jesus Vallejo anafanyiwa vipimo vya afya katika klabu ya Wolves kabla ya kuhamia klabuni hapo kwa  mkopo. (Talksport)

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.