Tetesi za soka Ulaya Julai 31, 2019

Tetesi za soka Ulaya Julai 31, 2019

31 July 2019 Wednesday 06:39
Tetesi za soka Ulaya Julai 31, 2019

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane anasema  hafahamu ikiwa mshambuliaji wa timu ya Colombia -James Rodriguez mwenye umri wa miaka 28 atakuwa kwenye klabu hiyo msimu ujao. (Marca)

West Brom hawajapokea ofa yoyote kutoka kwa Aston Villa ya kumsajili  winga wa uskochi Matt Phillips, mwenye umri wa miaka 28. (Birmingham Mail)

Meneja wa zamani wa Chelsea na Manchester United Jose Mourinho atarejea katika kazi hiyo wakati fursa itakapojitokeza. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Teddy Sheringham anasema Ole Gunnar Solskjaer anapaswa kumuuza kiungo wa kati Mfaransa Paul Pogba mwenye umri wa miaka 26. (Talksport)

Kipa wa Newcastle na England wa kikosi cha walio chini ya umri wa miaka -21 Freddie Woodman,ambaye ana umri wa miaka 22, anawindwa na Celtic na Arsenal, pamoja na klabu ambazo hazijatajwa . (Chronicle)

Manchester United wana nia kumsaini beki wa kati wa Barcelona na Ufaransa Samuel Umtiti, mwenye umri wa miaka 25. (Le10 Sport - in French)

Kiungo wa kati wa Atletico Madrid Koke anasema anaamini mshambuliaji wa Ureno Joao Felix mwenye umri wa miaka 19-atakuwa "mmoja wa wachezaji bora zaidi duniani . (ESPN)

Paris St-Germain wameweka ofa yao ya uhamisho wa mshambuliaji wao Neymar mwenye umri wa miaka 27 kwa Barcelona. (Marca) 

Arsenal wanakamilisha mkataba wa kumsajili mchezaji wa Celtic na Uskochi Kieran Tierney, mwenye umri wa miaka 22. (Mail)

Kiungo mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Mauro Icardi, mwenye umri wa miaka 26, uenda akajiunga Napoli kwa mkataba wa Yeuro milioni 80 (paundi milioni 73) . (Corriere dello Sport - in Italian)

Crystal Palace wameweka dau la takriban pauni milioni 14 kwa ajili ya mshambuliaji wa timu ya CSKA Moscow na Urusi -Fedor Chalov mwenye umri wa miaka 21 . (Sky Sports)

Mkurugenzi mkuu wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge anasema hakuelewa ni kwanini meneja Niko Kovac alisema kuwa klabu hiyo inaamini itasaini mkataba na winga Mjerumani Leroy Sane ambaye anaichezea sasa Manchester City akiwa na umri wa miaka 23. (Bild - in German)

Newcastle wamekataliwa dau la pauni milioni 4.5 ya usajili wa kiungo wa Amiens na Sweden Emil Krafth mwenye umri wa miaka 24 . (Sun)

Updated: 03.08.2019 07:32
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.