Tetesi za soka Ulaya Julai 7, 2019

Tetesi za soka Ulaya Julai 7, 2019

07 July 2019 Sunday 08:12
Tetesi za soka Ulaya Julai 7, 2019

TAJIRI wa klabu ya Everton, Farhad Moshiri anataka kumsajili mshambuliaji mwenye utata, Diego Costa (30)(Mail on Sunday) 

Manchester United ndio klabu iliyobakia katika kuwania saini ya beki wa kati wa Leicester City na England, Harry Maguire(26) lakini kikwazo ni kiwango kikubwa cha fedha ya usajili inachotaka Leicester cha paundi milioni 85. (Sun on Sunday)

Arsenal itamwinda winga wa Bournemouth na timu ya taifa ya  Scotland, Ryan Fraser, 25,   endapo  haitofanikiwa  kumsajili winga wa Crystal Palace's Wilfried Zaha. (Sunday Mirror)

Brentford  inataka kumsajili  mchezaji  beki wa Leeds United na timu ya taifa ya  Sweden, Pontus Jansson, 28. (BBC Radio Leeds)

Golikipa wa Ujerumani, Manuel Neuer, 33, anapanga kuitema klabu yake ya  Bayern Munich, taarifa hiyo imetolewa na  ajenta wake (Suddeutsche Zeitung - in German)

Beki Muingereza ,Danny Rose, 29,  ni miongoni mwa wachezaji tisa wanatazamia kutemwa na klabu ya  Tottenham. (Mail on Sunday) 
 
Ajenti wa kiungo wa timu ya Lazio, Mserbia, Sergej Milinkovic-Savic(24) amesafiri kuelekea Uingereza kufanya mazungumzo na klabu ya Manchester United . (Sport Mediaset - in Italian)

Beki wa kati wa Bournemouth na Uholanzi, Nathan Ake(24) anahitajika na klabu ya Man City  kwa paundi milioni 40 kama  mbadala wa Harry Maguire.(Sunday Mirror) 

Bournemouth  wamekubali kumsajili, beki wa kati, Muingereza Luton Town (23) kwa paundi milioni 4. (BBC)

Mshambualiji Mghana Jordan Ayew, 27, anatajiunga na Crystal Palace akitokea timu ya  Swansea kwa paundi milioni  2.5 mara baada ya mashindano ya Afcon 2019 kumalizika. (Guardian)

Mshambualiaji wa Manchester United na Ubelgiji  Romelu Lukaku anataka kuondoka klabuni hapo ili kujiunga na  klabu ya Juventus au Napoli. (Sun on Sunday)

Beki wa kushoto wa Real Betis na  timu ya Hispania chini ya miaka 21, Junior Firpo amevivutia vilabu vya Liverpool na Barcelona. (Muchodeportivo - in Spanish)

Benitez anataka kumchukua mshambuliaji wa timu ya taifa ya  Venezuela na timu ya Newcastle, Salomon Rondon(29)kwenda klabu yake mpya ya  Dalian Yifang ya China. (Mail on Sunday)

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.