Tetesi za soka Ulaya Julai 8, 2019

Tetesi za soka Ulaya Julai 8, 2019

08 July 2019 Monday 06:49
Tetesi za soka Ulaya Julai 8, 2019

MMILIKI wa klabu ya Newcastle  Mike Ashley anamtaka kocha wa timu ya Rangers, Steven Gerrard kuwa kocha wa timu yake.(Mirror)

Barcelona wameishinda klabu ya  Paris St-Germain katika kumsaini  kinda  wa miaka 16 mshambuliaji Muingereza, Louie Barry ambaye mkataba wake umemalizika kutoka klabu ya West Brom. (Sun)

Tottenham wapo katika mazungumzo ya kumuongezea mkataba wa muda mrefu beki wake, Ben Davies, 26 ambaye ni raia wa Wailes. (Telegraph)

Juventus wameaandaa paundi milioni 120 ili kurejesha tena klabuni hapo kiungo wa  Manchester United na Ufaransa, Paul Pogba. (Times)

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp  kupitia ajenti wake anasema atafundisha timu ya taifa ya Ujerumani (Welt - in German)

Burnley wanakamilisha mpango wa kumnyaka beki wa Stoke City, Eric Pieters(30). (Mail)

Beki wa zamani wa Uingereza na Asernal, Ashley Cole, 38, uenda akajumuisha katika benchi la ufundi la klabu ya Chelsea chini ya kocha mpya Frank Lampard. (Sun)

Kipa Mhispania, David de Gea, 28, anatarajia kusaini mkataba mpya na  Manchester United  atakuwa akilipwa paundi 350,000 kwa wiki. (Mirror)

Nottingham Forest wanakamilisha usajili wa kipa wa Manchester City,Mkosovo Aro Muric, 20,. (Telegraph)

Crystal Palace wanataka kumsajili beki wa Chelsea Reece James(19) kuziba nafasi iliyoachwa wazi na  Aaron Wan-Bissaka aliyejiunga   Manchester United . (Sun)

Updated: 08.07.2019 08:37
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.