Tetesi za soka Ulaya Julai 9, 2019

Tetesi za soka Ulaya Julai 9, 2019

09 July 2019 Tuesday 05:08
Tetesi za soka Ulaya Julai 9, 2019

Atletico Madrid wamefungua mazungumzo ya kisheria ya jinsi ya kumuadhibu mshambualiaji wake Mfaransa Antonie Griezmann(28) ambaye anatarajia kujiunga na Barcelona kwa dau la  paundi milioni 107.5. (Guardian)

Real Madrid wanakusudia kumuuza mshambuliaji Mcolombia, James Rodriguez (27) ili kuongeza fedha hadi paundi milioni 150 za kumnunua kiungo wa Man United na Ufaransa, Paul Pogba, 26. (Mail)

Napoli wanataka kumsajili mchezaji James Rodriguez kutoka   Real Madrid, pia klabu ya Napoli inamnyatia mshambualiaji  wa   Inter Milan, Muagentina, Mauro Icardi, 26. (Goal.com)

Bayern Munich  wanatarajia wiki ijayo winga wa kijerumani Leroy Sane, 23,  atafanya maamuzi ya kujiunga nao akitokea  Manchester City. (Mail)

Arsenal, Manchester United na Paris St-Germain wanapigana vikumbo kugombea saini ya kiungo wa Chelsea, Mfaransa Tiemoue Bakayoko, 24, (RMC Sport - in French)

West Ham wapo tayari kulipa paundi milioni 43.5 kumnyakua mshambuliaji  wa Celta Vigo  ya Hispania, Muuruguay, Maxi Gomez. Klabu ya Valencia nayo  inamtaka mchezaji huyo.(Sun)

Mshambuliaji wa Manchester United, Mbelgiji  Romelu Lukaku, 26, anamatumaini ya kujiunga na klabu ya Inter Milan Julai 20, 2019 . (Mirror)

Aston Villa  wameweka mezani paundi milioni  7 kumnyaka kipa wa  Burnley, Muingereza Tom Heaton, 33. (Sun)

Arsenal wapo katika hatua za mwisho kumsajili beki Mfaransa  na klabu ya Saint-Etienne William Saliba, mwenye umri wa miaka 18 kwa paundi milioni 25. (Evening Standard)

Liverpool wanampango wa kumtoa kwa mkopo   beki wake wa kushoto Muhispania,  Alberto Moreno(27) kwenda klabu ya Villarreal. (ESPN)

Gareth Bale(29) anatarajia kuanza mazoezi ya maandali na klabu yake ya  Real Madrid Jumatatu ijayo. (Marca)

Manchester City wapo katika hatua za mwisho kumsajili kiungo Muingereza anayechezea timu ya taifa chini ya miaka 17, Morgan Roger(16) kutoka klabu ya West Brom, (Mail)

Everton wametenga paundi milioni  35 ili kumnyaka mshambuliaji wa Kibrazil Malcom kutoka Barcelona . Pia Asernal nao wanamnyatia mchezaji huyo mwenye miaka 23 (RMC Sport - in French)

Watford wanataka kumsajili winga Mfaransa Allan Saint-Maximin, 22,  kutoka klabu ya  Nice  kwa ada ya paundi milioni 25  (Sky Sports)

Aston Villa bado wanataka kumbakisha kikosini kwa mkopo mchezaji beki, Axel Tuanzebe wa Manchester United. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 na anayechezea timu ya taifa ya Uingereza chini ya miaka 21. Ameichezea Villa mwaka jana kwa mkopo (Telegraph)

Sheffield United wameweka mezani paundi milioni 3  kumsajili kiungo wa Nottingham Forest ,Ben Osborn, 24. (Sun)

Updated: 09.07.2019 08:44
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.