Tetesi za soka Ulaya Juni 10, 2019

Tetesi za soka Ulaya Juni 10, 2019

10 June 2019 Monday 07:55
Tetesi za soka Ulaya Juni 10, 2019

West Ham ipo tayari kushindana na Arsenal na Tottenham kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Atalanta na timu ya taifa ya Ivory Coast Franck Kessie. Mchezaji huyo wa miaka 22 amekuwa akicheza kwa mkopo huko AC Milan tangu 2017. (Express)

Ombi la Man United limekataliwa  na Crystal Palace la thamani ya £40m kumsajili mchezaji wa timu ya taifa ya England ya wachezaji wa chini ya miaka 21 Aaron Wan-Bissaka. Timu hiyo ya Eagles inataka takriban £60m. (Sky Sports)

Mkufunzi wa Arsenal Unai Emery amefanya mazungumzo na beki wa kulia wa PSG na timu ya taifa ya Ubelgiji Thomas Meunier, mwenye umri wa miaka 27, kuhusu uwezekano wa kuhama msimu huu wa joto.(Express)


Tottenham itawasilisha ombi kwa Fulham kumwania winga wa timu ya taifa ya England ya wachezaji wasiozidi miaka 21 Ryan Sessegnon, mwenye umri wa miaka 19, msimu huu wa joto. (Football.London)

Chelsea imefufua hamu yake ya kutaka kumsajili winga wa Bayer Leverkusen na timu ya taifa ya Jamaica Leon Bailey, mwenye umri wa miaka 21, lakin ni lazima isubiri kuona iwapo marufuku iliyopewa ya uhamisho wa wachezaji itabatilishwa kabla ya kuwasilisha ombi hilo. (Mail)

Arsenal ina hamu ya kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Fiorentina Jordan Veretout, mwenye umri wa miaka 26, lakini mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa ya wachezaji wasiozidi miaka 21 tayari anafanya mazungumzo na Napoli. (L'Equipe)

Newcastle na Southampton zimewasilisha ombi kwa mshambuliaji wa Mainz na timu ya taifa ya Ufaransa ya wachezaji wasiozidi miaka 21 Jean-Philippe Mateta, aliye na miaka 21. (L'Equipe, kupitia Sport Witness)

Arsenal inataka kumsajili mlinzi wa Saint Etienne William Saliba, mwenye miaka 18, lakini timu hiyo ya Ligue 1 inataka kumchukua kwa mkopo msimu ujao wa joto. (Football.London)

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.