Tetesi za soka Ulaya Juni 11, 2019

Tetesi za soka Ulaya Juni 11, 2019

11 June 2019 Tuesday 08:50
Tetesi za soka Ulaya Juni 11, 2019

Barcelona wako tayari kutupa karata yao ya mwisho katika juhudi za kusaini mkataba na kiungo wa kati -nyuma wa Ajax na Uholanzi Matthijs de Ligt, mwenye umri wa miaka 19, wiki hii kwa kuanzisha upya mazungumzo na wakala wake Mino Raiola. (ESPN)

Paris St-Germain wanasema wanamatumaini makubwa ya kufikia makubaliano na Ajax kwa ajili ya kumleta kikosini De Ligt. (Mail)


Manchester City na Bayern Munich wanamgombea Rodri, mwenye umri wa miaka 22, ambaye ametangaza kuondoka Atletico Madrid, na amesema watamlipa malipo sawa na anayolipwa kiungo yeyote wa kati wa Uhispania  (AS - in Spanish)


Mlinda lango wa Atletico Madrid Jan Oblak anataka kuondoka katika timu hiyo msimu ujao, Mslovenia huyo (26), anapenda kwenda Manchester United zaidi ya Paris St-Germain. (ESPN)

Manchester United wameiambia Real Madrid kwamba kiungo wa kati Paul Pogba, mwenye umri wa miaka 26, hauzwi na wamekataa kutangaza bei ya mchezaji huyo Mfaransa. (AS)

Juventus wana nia ya kusaini tena mkataba na Pogba, lakini timu hiyo ya championi upande wa Serie A itatakiwa kuwauza wachezaji watano ili kuweza kummudu kiungo huyo wa kati wa United (Mail)

Manchester United wamekuwa wakishauriwa wamchukue beki wa kulia Muingereza Wan-Bissaka Aaron, licha ya dau la awali kwa ajili ya kijana huyo mwenye umri wa miaka 21- kukataliwa na Crystal Palace.  (Evening Standard)
United wako tayari kuongeza £50m kwa ajili ya Wan-Bissaka. (Mirror)

Manchester United huenda watathmini upya nia yao ya kusaini mkataba na mlinzi wa Tottenham Danny Rose, mwenye umri wa miaka 28, baada ya mchezaji huyo wa England kukiri kuwa anaweza kuondoka katika kikosi cha Spurs msimu huu. (Manchester Evening News)

Tottenham wanamtaka  kiungo wa nyuma  wa Marseille Mjapani Hiroki Sakai, ambaye ana umri wa miaka 29. (Sky Sports)

Manchester United wanakaribia kusaini mkataba na mshambuliaji wa Derby Country, Liam Delap, mwenye umri wa miaka 16- mtoto wake kiungo wa kati wa zamani wa Stoke Rory Delap. (Derby Telegraph)


Liverpool wameamua kuachana na azma yao ya kumsaini  mshambuliaji wa Werder Bremen-na timu ya taifa ya Ujerumani Max Kruse, mwenye umri wa miaka 31. (Liverpool Echo)


Mchezaji wa safu ya kati wa Ajax na Uholanzi Donny van de Beek, mwenye umri wa miaka 22, "ana malengo ya Primia Ligi " na angependa kujiunga na Manchester United au Tottenham msimu huu. (Talksport)

Valencia wanamtaka mshambuliaji wa Newcastle Muhispania Ayoze Perez, mwenye umri wa miaka 25. (Cope - in Spanish)

Chelsea wamefikiria kwa mara nyingine kusaini mkataba na beki  Mcrotia, Mateo Kovacic, mwenye umri wa miaka 25, kwa mkataba wa kudumu  kutoka Real Madrid. (Evening Standard)

Meneja wa timu ya Ufaransa Didier Deschamps amefichua kuwa  beki wa kushoto   wa Lyon Ferland Mendy, mwenye umri wa miaka 24, atajiunga na Real Madrid msimu huu. (Marca)

Beki wa kulia, Nelson Semedo, mwenye umri wa 25, anaweza kuondoka Barcelona msimu huu, huku Atletico Madrid wakimsaka,  Catalonia inamtaka kumuuza kwa bei ya kati ya Euro milioni 45 na milioni 50 mchezaji huyo (Marca)

Updated: 11.06.2019 10:57
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.