Tetesi za soka Ulaya Juni 12, 2019

Tetesi za soka Ulaya Juni 12, 2019

12 June 2019 Wednesday 08:05
Tetesi za soka Ulaya Juni 12, 2019

KIUNGO wa kati wa England Alex Oxlade-Chamberlain, mwenye umri wa miaka 25, anapanga kurefusha mkataba wake wa sasa na Liverpool hadi 2023. (Mail)


Real Madrid watafanya kila wawezalo kusaini mkataba na kiungo wa kati wa Manchester United Mfaransa Paul Pogba, mwenye umri wa miaka 26, kwani ndio chaguo la kwanza la Zinedine Zidane (Marca)


Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anaangalia uwezekano wa kupumzika kwa muda katika soka mwishoni mwa msimu ujao ikiwa atashinda Championi Ligi . (Star)

Manchester United wamefanya mawasiliano na kiungo wa kati wa Barcelona Mcroatian Ivan Rakitic (31). (Sport - in Spanish)

Man United wanataka kuvunja mikataba miwili na kuweka rekodi ya uhamisho wa mabeki kutoka England Aaron Wan-Bissaka, mwenye umri wa miaka 21, kutoka Crystal Palace na Harry Maguire, mwenye umri wa miaka 26, kutoka Leicester watakaolipwa pamoja pauni milioni 130. (Standard)


Mlinzi wa klabu ya Ajax ya Uholanzi Matthijs de Ligt, mwenye umri wa miaka 19, anasema " hajui moyo wake unasema nini " lakini ataamua juu ya hali yake ya baadae atakapokuwa mbali likizoni . (Mundo Deportivo - in Spanish)
Washauri wa De Ligt wamemwambia aende katika timu kama Manchester United ambako anakuwa na hakikisho la kuanza , kabla ya kuhamia Barcelona baadae katika taaluma yake (Sport)

Chelsea wameanzisha mazungumzo na meneja wa Derby Country, Frank Lampard  kurejea  Stamford Bridge kama mkufunzi wa timu hiyo.(Mail)

Man United wanataka sana kusaini mkataba na mchezaji wa timu ya England na Norwich City anayecheza safu ya ulinzi Max Aarons,mwenye umri wa miaka 19, ikiwa azma yao ya kumchukua Wan-Bissaka haitafanikiwa. (Sky Sports)

Chelsea wanataka Meneja atakayechukua nafasi ya Maurizio Sarri ambaye tayari anatarajia kuhamia katika klabu ya Italia ya Juventus baadae wiki hii. (Mirror)

West Ham wanamlenga mchezaji wa safu ya kati ya timu ya Villarreal ya Uhispania Pablo Fornals, mwenye umri wa miaka 23, Baada ya kutuliza haja yao kwa kiungo wa kati wa Celta Vigo Mslovakia Stanislav Lobotka, mwenye umri wa miaka 24. (Guardian)

Kipa Gianluigi Buffon, mwenye umri wa miaka 41, anaweza kujiunga na Porto baada ya kuondoka Paris St-Germain, kuchukua nafasi ya Spaniard Iker Casillas, mwenye umri wa miaka 38. (Tuttosport - in Italian)

Manchester United watamuhitaji mlindalango wa Ajax Mcameroon Andre Onana, mwenye umri wa miaka 23,ikiwa Muhispania David de Gea, mwenye umri wa miaka 28, ataondoka kikosini msimu huu. (Independent)

Barcelona wanatumai kujiingizia takriban Euro milioni 60 kutokana na mauzo ya wachezaji kabla ya Juni 30 kwa lengo la kuweka uwiano wa mahesabu ya akunti kwa ajili ya msimu wa 2018-19. (ESPN)

Washindi hao wa Ligi ya Uhispania wanamtaka mshambuliaji Louie Barry wa West Brom mwenye umri wa miaka 15 aliyeko katika kikosi cha Timu ya England ya walio na umri wa chini ya miaka 16. (Birmingham Mail 


Mshambuliaji wa timu ya Benfica ya Ureno Joao Felix, mwenye umri wa miaka 19, anataka kuhamia Atletico Madrid. (AS - in Spanish)

Manchester United wanafanya mazungumzo ya kumuuza beki Mtaliano Matteo Darmian, mwenye umri wa miaka 29, huku Valencia na klabu nyingine mbili za Italia  zikimtaka. (ESPN)

Updated: 14.06.2019 08:55
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.