Tetesi za soka Ulaya Juni 13, 2019

Tetesi za soka Ulaya Juni 13, 2019

13 June 2019 Thursday 06:48
Tetesi za soka Ulaya Juni 13, 2019


Manchester United watalazimika kuwa na euro milioni 150 ili kumzuia kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba (26), asiondoke . (Mirror)

Mazungumzo ya Arsenal kumsajili  mlinzi wa timu ya Ufaransa ya Saint-Etienne mwenye umri wa miaka 18 -William Saliba yamefika pazuri (Le10Sport - in French)

Mkurugenzi mtendaji wa Atletico Madrid -Miguel Angel Gil Marin amethibitisha kuwa mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann, mwenye umri wa miaka 28, atajiunga na Barcelona msimu huu. (Sport)

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amepuuza madai kuwa atakwenda mapumzikoni mwishoni mwa msimu ujao, endapo atachukua ubingwa wa klabu bingwa Ulaya.(Independent)
Mkurugenzi wa masuala ya mchezo wa Juventus Fabio Paratici amewasili jijini London kukamilisha mkataba kwa ajili ya Meneja wa Chelsea Muitaliano Maurizio Sarri. (Calciomercato)

Manchester United wamesitisha nia ya kumnunua mchezaji wa kimataifa wa Wales Gareth Bale(29) (Evening Standard)

Wakala wa Matthijs de Ligt Mino Raiola amekutana na Mkurugenzi wa mchezo wa Paris St-Germain Antero Henrique kuzungumzia juu ya uhamisho wa mchezaji huyo wa safu ya ulinzi ya Ajax na Uholanzi mwenye umri wa miaka 19 . Klabu zote zinakaribia kufikia mapatano ya euro milioni 75. (RMC Sport - in French)

PSG wamemtaka De Ligt asaini nao mkataba wa miaka mitano wa thamani ya euro milioni 12 kwa mwaka. (ESPN)


Tottenham wanamtaka mchezaji wa safu ya kati wa Lyon na Ufaransa Tanguy Ndombele, mwenye umri wa miaka 22, anatatizwa na thamani aliyopewa ya euro milioni 75. (guardian)

Chelsea hawatakuwa na chaguo la kumnunua Mcroatia anayecheza safu ya kati Mateo Kovacic kutoka Real Madrid. Badala yake kijana huyo mwenye umri wa miaka 25 amejipanga kurejea Inter Milan. (Mail)

AC Milan awanataka kusaini mkataba na kiungo wa kati-nyuma wa Liverpool Mcroasia Dejan Lovren, mwenye umri wa miaka 29. (Sky Sports)


Mchezaji wa safu ya mashambulizi wa Manchester United Romelu Lukaku,mwenye umri wa 26, amesema kuwa kuwa meneja wa Inter Milan Antonio Conte ni "meneja bora zaidi kuliko wote duniani" na kwamba, kando na upande wa Ligi ya Primia Serie A ni Ligi ambayo "amekuwa akiiota kila mara " kuichezea.Lakini hakujawa na mawasiliano baina yao . (ESPN)

Kiungo wa kati wa Arsenal raia wa Uruguay Lucas Torreira, mwenye umri wa mika 23,anasema kuwa hakuna mambo mengi yanayomfurahisha kimaisha England baada ya kuhama kutoka timu ya Italia ya Sampdoria msimu uliopita. (Ovacion, via Mirror)

Aston Villa wamejipanga kuwasilisha dau la euro milioni 14 kwa ajili ya muingereza Kalvin Phillips anayecheza katika safu ya kati katika klabu ya Leeds United akiwa na umri wa miaka 23.(Telegraph)

Updated: 15.06.2019 08:12
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.